WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, August 9, 2019

WAGENI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KWENYE MAONESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA

Wanafunzi wa Shule ya Awali na Msingi Modern ya Jijini Dodoma wakifurahia Siwa wakati walipotembelea banda la Bunge kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Jijini Dodoma hii leo. Kushoto ni Afisa Utafiti wa Ofisi ya Bunge Ndg. Aziza Makwai akiwasaidia Wanafunzi hao namna ya kubeba Siwa.

Afisa wa Bunge Ndg. Hosiana John akitoa Elimu kwa mgeni aliyetembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Afisa wa Bunge Ndg. Mohamed Salim akitoa Elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma walipotembelea banda la Bunge kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Jijini Dodoma hii leo.

Tuesday, August 6, 2019

MAAFISA WA BUNGE WATOA ELIMU KWA UMMA KWENYE MAONESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA

Afisa Sheria wa Bunge Ndg. Mossy Lukuvi akitoa Elimu kwa Wageni waliotembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Afisa Utafiti  wa Bunge Ndg. Aziza Makwai akitoa Elimu kwa mgeni aliyetembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.

Friday, August 2, 2019

WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE WAKUTANA KUCHAGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI BUNGENI

Watumishi wa Ofisi ya Bunge wakifuatilia jambo kwa makini Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma. 

Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Dodoma Ndg. John Mchenya akiongea na Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma. 

Mtumishi wa Ofisi ya Bunge Ndg. Frank Ngonyani akichangia jambo mbele ya kikao cha  Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma. 

Mtumishi wa Ofisi ya Bunge Bi. Jane Ndulesi akichangia jambo mbele ya kikao cha  Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge walipokuwa wakichagua Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo kwenye ukumbi wa Msekwa hii leo Jijini Dodoma.