Saturday, August 17, 2019
Friday, August 16, 2019
KAMATI YA PAC YAPEWA MAFUNZO NA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA
Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Ndg. Lightness Mauki akifafanua jambo alipokuwa akitoa Mada kuhusu Changamoto za usimamizi wa Matumizi ya Mashirika ya Umma nchini kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
|
Thursday, August 15, 2019
BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE LANDELEA NA KIKAO
Wednesday, August 14, 2019
SPIKA WA BUNGE AWATAKA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE KUFANYA KAZI KWA BIDII
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
amewataka watumishi wa Bunge kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa bidii.
Mhe. Spika alitoa rai hiyo kupitia
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson alipokuwa
anazindua Baraza la Wafanyazi la Ofisi ya Bunge lililofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Tunguu Zanzibar.
Alisema kunahitajika mabadiliko
katika utekelekezaji wa majukumu ya kila siku kwa watumishi katika kuchapa kazi
ili kuleta utendaji kazi wenye tija na ufanisi.
Aidha, aliwataka wajumbe kupitia
mada zitakazowasilishwa katika Mkutano huo wa Baraza kukumbuka wajibu wao
katika kutelekeza majukumu waliyopewa kulingana na taaluma husika na hatimaye
kufanikisha utekelezaji bora wa majukumu na madaraka ya Bunge Kikatiba.
Vilevile, alimpongeza Katibu wa
Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai kwa kufanikisha utatuzi wa changamoto ya muda
mrefu ya muundo wa Ofisi ya Bunge ambayo hatimaye ufumbuzi umewezesha kuundwa
kwa Baraza la Wafanyakazi.
“Naomba
nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wote mlioteuliwa na Tume ya Utumishi wa
Bunge kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na ni matumini yangu kwamba
mtatumia uwezo na karama mlizojaaliwa na Mwenyezi Mungu katika kutekeleza
majukumu yenu kwa ufanisi hivyo kuliwezesha Bunge kufikia malengo yake,” alisema.
Aliwapongeza pia Wajumbe na Wawakilishi
wa Idara na Vitengo kwa kuchaguliwa kushika nafasi hizo na kuwataka kutumia
nafasi zao ili kuwa kiungo kati ya Wafanyakazi wa kada, ngazi zote, Menejimenti
na Tume ya Utumishi wa Bunge.
Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi
ulihudhuriwa na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na
Afya, TUGHE Ndugu Hery Nkunda na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Ndugu John Mchenya
ambao walinasihi Baraza kudumisha ushirikiano na kuongeza ufanisi katika ujenzi
wa nchi.
Awali akizungumza katika mkutano
huo, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai alisema Ofisi ya Bunge imeunda
Baraza la Wafanyakazi baada kutokuwepo ya Baraza hilo katika kipindi kirefu
kutokana na changamoto zilizokuwepo za kimuundo za Ofisi ya Bunge.
Alisema, lengo la Baraza lililopo
kisheria ni kuboresha utendaji kazi wa
taasisi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na bila ya ugomvi wala mifarakano.
Kabla ya uzinduzi wa Baraza la
Wafanyakazi, wajumbe walimchagua Ndugu Frank Mbilinyi kuwa katibu wa Baraza na
Ndugu Felister Njovu kuwa Katibu
Msaidizi.
NAIBU SPIKA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano wa
Wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo
za Bunge, Tunguu Zanzibar pamoja na Ndugu Chacha Nyakega Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Ofisi ya Bunge na Ndugu Triphonia
Mng’ong’o Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu.
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo
za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo
za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai Mkataba kwa ajili ya kuunda
Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo.
Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Ndugu Hery Nkunda Mkataba kwa ajili ya
kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya uzinduzi. Uzinduzi huo umefanyika
katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma , Ndugu John Mchenya Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la
Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo. Uzinduzi huo umefanyika
katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
| Wajumbe wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja |
Saturday, August 10, 2019
Friday, August 9, 2019
WAGENI MBALIMBALI WATEMBELEA BANDA LA BUNGE KWENYE MAONESHO YA NANENANE JIJINI DODOMA
![]() |
Wanafunzi
wa Shule ya Awali na Msingi Modern ya Jijini Dodoma wakifurahia Siwa wakati
walipotembelea banda la Bunge kwenye Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Jijini
Dodoma hii leo. Kushoto ni Afisa Utafiti wa Ofisi ya Bunge Ndg. Aziza Makwai akiwasaidia Wanafunzi hao namna ya kubeba Siwa.
|
![]() |
Afisa wa Bunge Ndg. Hosiana John akitoa Elimu
kwa mgeni aliyetembelea banda la Bunge hii leo kwenye Maonesho ya Wakulima ya
Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma.
|
![]() |
Afisa wa Bunge Ndg. Mohamed Salim akitoa Elimu
kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma walipotembelea banda la Bunge kwenye
Maonesho ya Wakulima ya Nanenane Jijini Dodoma hii leo.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)



