Friday, April 22, 2022
Tuesday, April 5, 2022
SPIKA DKT. TULIA AFUNGUA MAFUNZO WAKATI WA KUWASILISHWA KWA TAARIFA JUU YA UCHAFUZI WA MTO MARA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akifungua Mafunzo wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa juu ya kuchafuka kwa Mto Mara na Hatua zilizochukuliwa leo Aprili 5, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma. Taarifa hiyo imewasilishwa na Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Seleman Jaffo. Kushoto ni Waziri Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. David Mwakiposa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akifungua Mafunzo wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa juu ya kuchafuka kwa Mto Mara na Hatua zilizochukuliwa leo Aprili 5, 2022 mbele ya Waheshimiwa Wabunge katika Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. David Mwakiposa
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishiriki Mafunzo wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa juu ya kuchafuka kwa Mto Mara na Hatua zilizochukuliwa leo Aprili 5, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma. Taarifa hiyo imewasilishwa na Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Seleman Jaffo
SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ALGERIA NCHINI
SPIKA DKT. TULIA AKIMUAPISHA MBUNGE WA KUTEULIWA MHE. SHAMSI VUAI NAHODHA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akimuapisha Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha leo Aprili 5, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Monday, April 4, 2022
KATIBU NENELWA VIKAO VYA BUNGE KURUSHWA LIVE
Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 4, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
Katika mazungumzo hayo Katibu Nenelwa alisema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge, Kamati ya Uongozi ya Bunge imeridhia Vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 5 Aprili, 2022 wakati wa Mkutano wa 7 wa Bunge ambao ni mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali.
SPIKA DKT. TULIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI SIMBACHAWENE
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Bunge, Sera na Uratibu, Mhe. George
Simbachawene baada ya kumtembelea kwa lengo la kujitambulisha kwake katika
Ofisi ya Spika iliyopo Bungeni Jijini Dodoma leo Aprili 4, 2022
Friday, April 1, 2022
SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA BAJETI CHA KUPOKEA MASUALA MUHIMU YALIYOJITOKEZA KWENYE KAMATI ZA KISEKTA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo
Viongozi Mbalimbali wa Serikali na Bunge wakishiriki kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge,
Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc pamoja na Mkurugenzi
wa Kamati za Bunge, Ndg. Athuman Hussein wakishiriki kikao cha Kamati ya
Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye
Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha
2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika
Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.
