WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, July 11, 2017

MAKAMISHINA WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA UGANDA WAKUTANA NA MAKAMISHINA WA TUME YA UTUMISHI WA BUNGE LA TANZANIA


Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge Mhe Mussa Azzan Zungu  akiongoza kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Kikao baina ya Makamishina hao ambacho lengo kubwa lilikuwa ni kubadilishana uzoefu wa utedaji kazi kiliongozwa na Mhe Zungu  kwa niaba ya Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania. Makamishina hao wa Bunge la Uganda wapo nchini kwa ziara ya Kibunge ya siku mbili.

 Kikao kikiendelea
Kiongozi wa Msafara Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda Mhe Cecilia  Ogwal (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Bunge mbaye pia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania Dkt. Thomas Kashililah akizungumza wakati wa  kikao baina ya Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

 Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Uganda  na Makamishina wa Tume ya Utumishi wa Bunge la Tanzania  (waliokaa) na baadhi ya Watumishi wa pande zote mbili katika  picha ya pamoja mara baada ya kikao.

Thursday, July 6, 2017

SPIKA WA BUNGE APOKEA MSAADA WA MIFUKO MIA MBILI YA SEMENTI NA HUNDI YA SH. MILIONI 15 KUTOKA BENKI YA CRDB TAWI LA DODOMA KWA AJILI YA UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU, WILAYANI KOGWA, DODOMA.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  (katikati) akipokea   hudi ya shilingi  milioni 15 na msaada wa  Mifuko mia mbili (200) ya sementi kutoka   kwa Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi  (kushoto) waliotoa ili kusaidia ujenzi wa nyumba za Walimu  wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Wilayani Kogwa, Dodoma wengine katika picha ni wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Dodoma


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) akionyesha  hudi ya shilingi  milioni 15 aliyokabidhiwa na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi (kushoto) alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu  wa Shule ya sekondari Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma kulia  ni Mkuu wa Shule hiyo Ndg. Msafiri Simon.


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza mara baada ya kukabidhiwa    hudi ya shilingi  milioni 15 na Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi alipokuwa wanatoa msaada wa ujenzi wa nyumba za Walimu  wa Shule ya sekondari Laikala, Kogwa, Dodoma. Walioshikilia hundi hiyo ni Wanafunzi wa shule hiyo


Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Walimu, Wanafunzi wa shule ya Laikala iliyopo Kogwa, Dodoma na wakazi Kata ya Saranga (hawapo pichani), mara baada ya kupokea msaada huo kushoto ni Mkurugenzi wa CRDB Benki Tawi la Dodoma Ndg. Rehema Hamisi na kulia Diwani wa kata ya Sagara Ndg. Simon Kamando.

Wednesday, July 5, 2017

BUNGE LAAHIRISHWA HADI SEPTEMBA 5

Mkutano wa Saba wa Bunge umeahirishwa hadi Septemba 5 mwaka huu huku Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwapongeza Wabunge na Mawaziri kwa ushirikianio wao katika kipindi chote cha miezi mitatu.

Akitoa shukrani hizo mara baada ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kutoa hoja ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa Spika aliwashukuru pia wasaidizi wake ambao ni Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na wenyeviti wa tatu wa Bunge.

“Vilevile kwa niaba ya wabunge wote, tunamshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutuwezesha kuhakikisha Bunge hili linaendelea, Miswada tunayoipitisha hapa anaipitisha kwa haraka bila kusita, tunaenedelea kufanya kazi na Serikali yake ambayo iko hapa,” alisema

“Shukrani kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye yupo hapa Bungeni, ametupa kila aina ya ushirikiano, shukrani pia kwa mawaziri wote, Kambi Rasmi ya Upinzani kwa changamoto mnazotupatia ambazo zimetusaidia kuendesha shughuli, shukrani kwa Kamati ya Uongozi na Kamati nyingine zote” alisema.

Awali akitoa hotuba ya kuahirisha Bunge, Mheshimiwa Majaliwa alisema Katika Mkutano huu wa Bunge, Bunge lilijadili na kupitisha Bajeti za Wizara zote 19 pamoja na Bajeti Kuu ya Serikali.

Aidha, alisema Bunge limepitisha miswada mbalimbali pamoja na Maazimio matano ya kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa na kwamba pia lilipitisha Azimio la Bunge kumpongeza Rais Dkt. John Magufuli kwa hatua anazochukua za kukabiliana na upotevu wa mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini.

“Katika Mkutano huu jumla ya maswali 499 ya msingi na mengine 1,834 ya nyongeza yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali kupitia kwa Waheshimiwa Mawaziri, Manaibu Mawaziri na maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu,” alisema.

Alisema pia Bunge liliendesha semina mbalimbalimbai kwa waheshimiwa Wabunge kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi na kuwapa uelewa mpana wa masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Nchi.

“Bunge pia lilipata fursa ya kuchagua wawakilishi wa Tanzania kwenye Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Wabunge tisa walichaguliwa

Aidha, aliwataka Watanzania kuendelea kulinda na kudumisha amani nchini ili wananchi waweze kushiriki shughuli za maendeleo bila hofu

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, ulinzi na usalama, afya, ardhi pamoja na masuala mbalimbali kuhusiana na Serikali za Mitaa