WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, September 12, 2018

WAGENI KUTOKA SEHEMU MBALIMBALI WAENDELEA KUTEMBELEA BUNGE

Maseneta kutoka Bunge la Ufaransa wakifuatilia Mjadala wa Bunge katika Kikao kilichoendelea hii leo Jijini Dodoma, kutoka kulia ni Mkuu wa msafara huo Seneta Ronan Dantec, Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Frederic Clavier, Seneta Cyril Pelleh pamoja na Seneta Bernard Jomier.

Sehemu ya Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Jitegemee ya Jijini Dar es salaam wakifuatilia Mjadala wa Bunge katika Kikao cha Bunge kilichoendelea hii leo Jijini Dodoma.

Tuesday, September 11, 2018

WABUNGE WANAWAKE WAPEWA SEMINA YA UONGOZI JIJINI DODOMA

Mtoa Mada kwenye Semina ya masuala ya Uongozi kwa Wabunge Wanawake Ndg. Venance Shillingi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akifafanua jambo katika semina hiyo iliyofanyika hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.
Sehemu ya Wabunge Wanawake wakifuatilia kwa karibu maelezo kutoka kwa Mtoa Mada katika Semina ya masuala ya Uongozi iliyotolewa kwa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania.
Katibu wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) Mheshimiwa Loresia Bukwimba akichangia jambo katika Semina ya masuala ya Uongozi iliyotolewa kwa Wabunge Wanawake kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.

Mjumbe wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG) Mheshimiwa Shally Raymond akichangia jambo katika Semina ya masuala ya Uongozi iliyotolewa kwa Wabunge Wanawake kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo.

Saturday, September 8, 2018

SPIKA ASHIRIKI MAFUNZO YALIYOANDALIWA NA BENKI KUU KWA AJILI YA WABUNGE WOTE

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila akizunugumza katika Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa Wabunge wote yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George Simbachawene akifuatilia kwa makini maelezo ya Mtoa Mada katika Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.


Sehemu ya Wabunge wakifuatilia Mafunzo yaliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa Wabunge wote yaliyofanyika hii leo katika Ukumbi wa Pius Msekwa Jijini Dodoma.