
Tuesday, December 6, 2022
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti ya Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Daniel Sillo wametembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) na kukutana na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge hilo kwa lengo la kubadilishana mawazo katika masuala mbalimbali ya kibajeti
Monday, December 5, 2022
Friday, November 25, 2022
WACHEZAJI TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB WASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA MICHEZO YA MABUNGE YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI NCHINI SUDAN KUSINI
Matukio katika picha
yaliyojiri leo tarehe 25 Novemba, 2022 wakati wachezaji wa timu ya Bunge Sports
Club wakishiriki katika uzinduzi wa Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki katika Ukumbi wa Freedom Hall, Juba Nchini Sudan Kusini.
Kauli Mbiu ya Michezo hiyo
ni Kupanua na Kuimarisha Muungano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Kuongeza umoja
wa Wananchi wake kupitia Michezo.
Wednesday, November 23, 2022
WACHEZAJI WA BUNGE SPORTS CLUB WAWASILI SUDAN KUSINI KUSHIRIKI MASHINDANO YA MICHEZO YA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu kwa niaba ya Spika wa Bunge akiwakabidhi bendera ya Bunge Wachezaji wa Bunge Sports Club wanaoelekea nchini Sudan Kusini kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukio la kuwaaga Wachezaji hao limefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu akizungumza wakati akiwaaga kwa niaba ya Spika wa Bunge Wachezaji wa Bunge Sports Club wanaoelekea nchini Sudan Kusini kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukio la kuwaaga Wachezaji hao limefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bunge Sports Club, Mheshimiwa Tarimba Abbas akizungungumza wakati wakuwaaga Wachezaji wa Bunge Sports Club wanaoelekea nchini Sudan Kusini kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tukio la kuwaaga Wachezaji hao limefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Juba nchini Sudan kwa ajili ya kushiriki katika michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
....................................................................................
Wachezaji wa Timu ya Bunge Sports Club wamewasili Jijini Juba nchini Sudan Kusini kwa ajili ya kushiriki katika mashidano ya michezo ya 12 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inayotarajiwa kuanza tarehe 25 Novemba hadi 2 Disemba 2022.
Awali Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu aliwakabidhi Wachezaji hao bendera ya Taifa na Bunge kwa niaba ya Spika wa Bunge. Tukio hilo lilifanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Aidha akizungumza na Wachezaji hao kabla ya kuwakabidhi bendera Naibu Spika aliwaasa kudumisha heshima ya taifa pamoja na nidhamu wakati wote wa mashidano.
"Nendeni mkadumishe heshima ya taifa letu na mkalitangaze, kama taifa tuna fursa mbalimbali zikiwemo za utalii," alisema Naibu Spika.
Pia Naibu Spika aliwaambia wachezaji hao kwamba wanatarajiwa kurudi na vikombe katika michezo mbalimbali ambayo watashiriki.




























