WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, August 31, 2017

CAG atoa semina kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti

 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akiwasilisha mada kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika semina iliyohusu Ripoti za CAG  kuhusu kaguzi za taarifa za fedha kwa mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2016. Semin hiyo imefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad akiwasilisha mada kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika semina iliyohusu Ripoti za CAG  kuhusu kaguzi za taarifa za fedha kwa mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2016

Wednesday, August 30, 2017

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA CHUO CHA KODI NA CHUO CHA UHASIBU

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo cha Kodi wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara katika chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika katika mkutano na Menejimenti ya Chuo cha Kodi wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kutembelea Chuo hicho kwa lengo la kuangalia utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu (TIA)  cha Jijini Dar es Salaam, Dkt. Joseph Kihanda akisoma taarifa ya utekezaji wa majukumu ya Chuo hicho kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara chuoni hapo

Tuesday, August 29, 2017

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM)

Wajumbe wa Kamati ya  Bunge ya Bajeti wakiwa kwenye kikao na Menejimenti ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  wakati walipofanya ziara  kutembelea Chuo hicho.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doroth Mwanyika akijibu hoja mbalimbali za Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakati wajumbe hao walipotembelea Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Prof. Lettice Rutashobya na Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia.

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WATEMBELEA MRADI WA MABASI YA MWENDOKASI KUANGALIA MFUMO WA UKUSANYAJI NAULI



Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Hawa Ghasia akielekezwa jinsi ya kutumia risiti ya Mwendokasi kwa ajili ya kuingia kituoni kusubiri basi.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa ndani ya Basi la Mwendo Kasi wakielekea Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam, wajumbe hao walikuwa wakikagua mfumo wa kukusanya fedha za nauli kwa mabasi hayo uliotengenezwa na Kampuni ya Maxcom.