Thursday, September 28, 2017
Thursday, September 21, 2017
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichokaa kumhoji Mbunge wa Kigoma Mjini Mheshimiwa Zitto Kabwe kufuatia kutoa matamshi yanayolidharirisha Bunge kupitia mitandao ya Kijamii. |
Wednesday, September 20, 2017
Thursday, September 14, 2017
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mradi wa Kulijengea
uwezo Bunge LSP akitoa neno la Shukran kwa Wafadhili wa Mradi wa Awamu ya Pili
wa Kulijengea uwezo Bunge LSP II unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa UNDP katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.
|
Katibu
wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akitoa tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa
Kulijengea uwezo Bunge LSP I katika hafla ya uzinduzi wa Mradi huo
kwa Awamu ya Pili LPS II 2017-2021 iliyofanyika leo Bungeni Mjini Dodoma.
|
Wednesday, September 13, 2017
Tuesday, September 12, 2017
SPIKA WA BUNGE AHUDHURIA HAFLA YA UZINDUZI WA MPANGO WA WIZARA YA FEDHA
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai akitoa salamu kwa wajumbe waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa maboresho wa sekta ya fedha kwa taasisi za umma (PFMRP) awamu ya tano 2017/18 mpaka 2021/22 katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Yustino Ndugai akipokea kitabu cha mpango mkakati wa Wizara ya Fedha na Mipango wa miaka mitano wa maboresho ya sekta ya fedha kwa taasisi za umma (PFMRP) awamu ya tano 2017/18 mpaka 2021/22 katika hafla iliyofanyika leo mjini Dodoma. |
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar amtembelea Spika wa Bunge Mjini Dodoma
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifurahi
jambo wakati akimsikiliza Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa
Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma.
|
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahi katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma na Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu |
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai (wa kwanza kulia) akifurahi katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Zuberi Ali Maulid alipomtembelea ofisini kwake, Bungeni Mjini Dodoma na Mheshimiwa Jenista Mhagama Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Watu wenye Ulemavu |
Saturday, September 9, 2017
PROFESA MAKAME MBARAWA AWASILISHA MAELEZO YA MUSWADA WA SHERIA YA RELI WA MWAKA 2017 KWA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu,
Mheshimiwa Rashid Chuachua akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo
kilichokutana kwa ajili ya kusikiliza maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria
ya Reli wa mwaka 2017, Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Profesa Makame Mbarawa.
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa akiwasilisha maelezo ya Muswada wa Sheria ya Reli wa mwaka 2017 kwa
Kamati ya Bunge ya Miundombinu, kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Mheshimiwa Rashid Chuachua.
|
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwasilisha maelezo
kuhusu Muswada waSheria ya Reli wa mwaka 2017 ambao umeshasomwa Bungeni kwa
mara ya kwanza.
|
Friday, September 8, 2017
Thursday, September 7, 2017
RAIS DKT MAGUFULI APOKEA TAARIFA MBILI ZA KAMATI ZA BUNGE ZA KIUCHUNGUZI WA BIASHARA YA MADINI YA TANZANITE NA ALMASI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli akipokea toka kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim
Majaliwa ripoti mbili za Kamati Maalum za Bunge zilizofanya uchunguzi wa Biashara ya
Madini ya Almasi na Tanzanite hapa nchini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli akizungumza mara baada
ya kupokea ripoti mbili za Kamati
Maalum za Bunge zilizofanya uchunguzi wa
Biashara ya Madini ya Almasi na Tanzanite Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti za kiuchunguzi za Biashara ya Madini ya Tanzanite na Almasi kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza wakati wa kukabidhi ripoti za kiuchunguzi za Biashara ya Madini ya Tanzanite na Almasi kwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini
Dar es Salaam
Mwenyekiti
wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya
uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Tanzanite hapa nchini Mheshimiwa Dotto Biteko akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya
uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi hapa nchini Mheshimiwa Mussa Azzan
Zungu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi ripoti hiyo kwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Mheshimiwa John Pombe Magufuli (katikati),
katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu Mheshimiwa
Kassim Majaliwa (wa pili waliokaa kushoto) na Spika wa
Bunge Job Ndugai (wa pili waliokaa kulia), Mweyekiti wa
Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya
uchunguzi wa Biashara ya Madini ya Almasi hapa nchini Mhe Mussa Azzan Zungu (wa kwanza kulia waliokaa) na Mweyekiti wa Kamati Maalum ya Bunge iliyofanya uchunguzi wa
Biashara ya Madini ya Tanzanite hapa nchini Mhe Dotto Biteko (wa kwanza kushoto waliokaa) na Wajumbe wa
Kamati zote mbili (waliosimama) mara baada ya kuzipokea ripoti hizo Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Posts (Atom)