WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, March 26, 2020

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAJADILI BAJETI YA SEKTA YA UCHUKUZI


Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mheshimiwa Isack Kamwelwe akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu ambapo Wizara yake  imewasilisha Taarifa ya utekeleaji ya bajeti ya sekta ya uchukuzi  kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakiwa katika kikao cha kamati ambapo wamepokea na kujadili Taarifa ya utekeleaji ya bajeti ya sekta ya uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.


Wednesday, March 11, 2020

WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO DKT. PHILIP MPANGO AMEWASILISHA MAPENDEKEZO YA SERIKALI YA MPANGO WA MAENDELEO YA TAIFA NA KIWANGO NA UKOMO WA BAJETI KWA MWAKA 2020/2021 KATIKA MKUTANO WA WABUNGE WOTE ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MSEKWA JIJINI DODOMA.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa maelezo ya awali kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kuwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021.katikati ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Dkt. Mpango, tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021. tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akitoa maelezo ya awali kabla ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kuwasilisha Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021.katikati ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Dkt. Mpango na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson, tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai (mwenye miwani) pamoja na baadhi wa mawaziri na wabunge wakifuatilia uwasilishwaji wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa na Kiwango na Ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/2021 uliofanywa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango. tukio hilo limefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma

Sunday, March 8, 2020

WAFANYAKAZI WA BUNGE WAPATIWA MAFUNZO KUHUSIANA NA MAADILI NA UTUNZAJI WA SIRI


Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai amefungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Bunge, kuhusu maadili, utunzaji wa siri mahala pa kazi, UKIMWI na ugonjwa wa Korona.Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai amefungua mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Bunge, kuhusu maadili, utunzaji wa siri mahala pa kazi, UKIMWI na ugonjwa wa Korona.Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma.

Wafanyakazi wa Bunge wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.

Wafanyakazi wa Bunge wakifuatilia mada katika mafunzo hayo. 

Wednesday, March 4, 2020

KAMATI YA BUNGE MASUALA YA UKIMWI YATEMBELEA GEREZA LA ARUSHA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo walipomtembelea ofisini kwake leo Machi 4
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya wakifuatilia kwa makini uwasilishwaji wa taarifa ya Gereza Kuu Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Oscar Mukasa atembelea Gereza Kuu la Arusha na kupokea taarifa ya hali ya wafungwa wanaoishi na virusi vya Ukimwi.