WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, April 27, 2022

SPIKA DKT. TULIA ASHIRIKI ZOEZI LA KUUAGA MWILI WA MHE. IRENE NDYAMKAMA

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akishiriki zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mhe. Irene Alex Ndyamkama leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akishiriki zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mhe. Irene Alex Ndyamkama leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.


Katibu wa Bunge, Mhe. Nenelwa Mwihambi, ndc akishiriki zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mhe. Irene Alex Ndyamkama leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.



 Waheshimiwa Wabunge wakishiriki zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa, Mhe. Irene Alex Ndyamkama  leo Aprili 27, 2022 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Tuesday, April 5, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFUNGUA MAFUNZO WAKATI WA KUWASILISHWA KWA TAARIFA JUU YA UCHAFUZI WA MTO MARA






Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akifungua Mafunzo wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa juu ya kuchafuka kwa Mto Mara na Hatua zilizochukuliwa leo Aprili 5, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma. Taarifa hiyo imewasilishwa na Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Seleman Jaffo. Kushoto ni Waziri Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe.  David Mwakiposa Kihenzile



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akifungua Mafunzo wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa juu ya kuchafuka kwa Mto Mara na Hatua zilizochukuliwa leo Aprili 5, 2022 mbele ya Waheshimiwa Wabunge katika Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Seleman Jaffo na Mwenyekiti wa Bunge, Mhe.  David Mwakiposa Kihenzile


 


 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishiriki Mafunzo wakati wa kuwasilishwa kwa taarifa juu ya kuchafuka kwa Mto Mara na Hatua zilizochukuliwa leo Aprili 5, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bunge Jijini Dodoma. Taarifa hiyo imewasilishwa na Kamati Maalum iliyoundwa na Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Seleman Jaffo


SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ALGERIA NCHINI


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akizungumza na Balozi wa Algeria Nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal leo Aprili 5, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Algeria Nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal leo Aprili 5, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.


 

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Algeria Nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal leo Aprili 5, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akiagana na Balozi wa Algeria Nchini Tanzania, Mhe. Ahmed Djellal leo Aprili 5, 2022 ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

SPIKA DKT. TULIA AKIMUAPISHA MBUNGE WA KUTEULIWA MHE. SHAMSI VUAI NAHODHA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akimuapisha Mbunge wa kuteuliwa, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha leo Aprili 5, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. 

Monday, April 4, 2022

KATIBU NENELWA VIKAO VYA BUNGE KURUSHWA LIVE



 Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza na Waandishi wa habari leo Aprili 4, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.

Katika mazungumzo hayo Katibu Nenelwa alisema baada ya maboresho ya Studio ya Bunge, Kamati ya Uongozi ya Bunge imeridhia Vikao vya Bunge vitaanza kurushwa live kuanzia kesho tarehe 5 Aprili, 2022 wakati wa Mkutano wa 7 wa Bunge ambao ni mahsusi kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Serikali.

SPIKA DKT. TULIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI SIMBACHAWENE


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Bunge, Sera na Uratibu, Mhe. George Simbachawene baada ya kumtembelea kwa lengo la kujitambulisha kwake katika Ofisi ya Spika iliyopo Bungeni Jijini Dodoma leo Aprili 4, 2022


Friday, April 1, 2022

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI NA KAMATI YA BAJETI CHA KUPOKEA MASUALA MUHIMU YALIYOJITOKEZA KWENYE KAMATI ZA KISEKTA


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Daniel Sillo


Viongozi Mbalimbali wa Serikali na Bunge wakishiriki kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc pamoja na Mkurugenzi wa Kamati za Bunge, Ndg. Athuman Hussein wakishiriki kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi na Kamati ya Bajeti cha kupokea Masuala muhimu yaliyojitokeza kwenye Kamati za Kisekta wakati wa kujadili Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 leo Aprili 1, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.