Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua kwa niaba ya Spika wa Bunge Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua kwa niaba ya Spika wa Bunge Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa (kushoto), Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (katikati) na Mheshimiwa Deus Sangu (kulia) wakimsikiliza Naibu wa Spika Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Mhe. Najma Giga (kushoto) na Mhe. Shamsia Mtamba (kulia) wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akizungumza na Katibu Mkuu wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Balozi Onyango Kakoba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Sudan Kusini ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge laUganda ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), (katikati) katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) mara baada ya kufngua Mkutano wa vikao vya Kamati za Jukwaa hilo katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika atoa Wito wa Kudumisha amani kwa Nchi za Maziwa Makuu
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), amefungua kwa niaba ya Spika wa Bunge Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo, Mhe. Zungu ametoa wito kwa wakuu wa nchi za ukanda wa maziwa makuu, kudumisha umoja na amani kwa kuwa kwani njia ndio njia kuu itakayosaidia katika kuwalinda raia na pia kukuza uchumi wa ukanda huo.
Alisema migogoro katika baadhi ya nchi za ukanda wa Maziwa Makuu una athari kubwa si tu kwa nchi husika lakini pia kwa nchi jirani.
Aliongeza kuwa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia, inaamini kuwa amani ndio msingi pekee wa maendeleo.
“Wazo letu la msingi ni kwamba amani, usalama na maendeleo haviwezi kutenganishwa, watu wetu wanaweza kufanikiwa iwapo nchi itakuwa na amani,” alisema.
Alisema ustawi wa kiuchumi, kijamii na kimazingira unahitaji kiasi kikubwa cha ushirikiano na uaminifu ndani ya jamii na bila amani na usalama hakuwezi kuwa na maendeleo endelevu.
“Eneo letu hili la maziwa makuu tuna watu takribani milioni 312 na tuna GDP ya bilioni 325 ni uchumi mkubwa sana. Tukiamua kuwa na amani tutasaidia wananchi wetu, tukiamua kupigana watanufaika wanaoleta ugomvi, wengi tuliobaki tutaumia,” alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo, Balozi Onyango Kakoba alisema ni wakati muafaka sasa kwa Viongozi wote wa kanda hiyo kufanya kazi ya kusaidia kuleta amani Mashariki mwa Congo na Sudan kwani hali hiyo inaleta athari kubwa kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Jukwaa hilo lina nchi wanachama 12 ambazo ni Burundi, Kenya, Rwanda, Sudan Kusini, Uganda, Angola, Tanzania, DRC, Jamhuru ya Kongo, Jamhuri ya Kati, Zambia na Sudan.
Kamati za Jukwaa hilo zinazotarajiwa kufanya vikao kwa nyakati tofauti ni Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Demokrasia na Utawala Bora.