Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC),Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa ameambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia vifaa vya matibabu katika Jengo la Dharula la Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Moan Simiyu wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua jengo hilo.
Tuesday, March 26, 2024
KAMATI YA LAAC IMEIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASWA MKAONI SIMIYU KWA UTEKELEZAJI MZURI WA MRADI WA JENGO LA DHARULA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA HIYO NA UJENZI WA KIWANDA CHA KUTENGENEZA CHAKI
Sunday, March 24, 2024
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MRADI WA SHULE YA SEKONDARI NA ZAHANATI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA
Saturday, March 23, 2024
KAMATI YA BUNGE YA LAAC IMETEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI MKOANI MARA
Friday, March 22, 2024
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MRADI WA SOKO NA JENGO LA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME
Thursday, March 21, 2024
WAJUMBE WA KAMATI YA LAAC WAMETEMBELEAA NA KUKAGUA MIRADI MIWILI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA TARIME
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiangalia mchoro wa ramani ya Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula pomoja na Mjumbe wa Kamati Mheshimiwa Suma Fyandomo wakiangalia ujenzi wa maabara ya kemia kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari iliyopo Kijiji cha Nyasaricho katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.
NAIBU SPIKA ZUNGU AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA URUSI NCHINI
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb),
akisalimiana na Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Andrey Avetisyan alipomtembelea
tarehe 20 Machi, 2024 katika ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa
Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), akizungumza na Balozi wa Urusi nchini, Mhe.
Andrey Avetisyan alipomtembelea tarehe 20 Machi, 2024 katika ofisi ndogo za
Bunge Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa
Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), akimpatia zawadi Balozi wa Urusi nchini,
Mhe. Andrey Avetisyan alipomtembelea tarehe 20 Machi, 2024 katika ofisi
ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
KATIBU NENELWA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE
Katibu wa Bunge
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa
Mwihambi, ndc akiongoza kikao cha
Baraza hilo kilichofanyika tarehe 20 Machi, 2024 katika ofisi za Bunge Jijini
Dodoma.
Tuesday, March 19, 2024
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MIRADI MITATU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA GEITA
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Munde Tambwe akizungumza kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika zahanati ya Bulela iliyopo Halmashauri ya Mji wa Geita, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati,Mheshimiwa Stansalaus Mabula na kushoto ni mjumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Daimu Mpakate.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC),Mheshimiwa Stansalau Mabula akiambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua mradi wa ujenzi wa mpira wa miguu Geita katika Halmashauri ya Mji wa Geita.
Monday, March 18, 2024
KAMATI YA PAC YAKAGUA MRADI WA KUTOA MAJI ZIWA VIKTORIA NA KUSAMBAZA KATIKA MIJI YA TABOTA, IGUNGA NA NZEGA
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kupokea maji kutoka Ziwa Viktoria na kusambaza katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega uliotekelezwa na Wizara ya Maji.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb) wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo na baadae kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya Kwanza na ya pili.
Alisema Kamati inaipongeza TUWASA kwa kusimamia vizuri mradi huo na kufikia malengo ya Serikali ya kufikisha maji safi na salama kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa ukame ambayo hayana vyanzo vya maji vya uhakika.
“TUWASA mmejitahidi sana, kwa macho tumejionea ubora wa miundombinu, sasa katika uendelevu wa mradi mlioueleza jitahidini na maeneo yaliyobakia ya Sikonge, Urambo Isikizya, kaliua, Shelui na Tinde maji yawafikie wananchi.” Alisema
Mheshimiwa Hasunga aliwasisitiza TUWASA kuhakikisha wanaongeza umakini na usimamizi wa miundombinu ya mradi huo kwa lengo la kuondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huo.
“Kwenye changamoto ya upotevu wa maji tutaendelea kupambana, ongezeni usimamizi ili maji yasipotee yawafikie wananchi.” Alisema
Mapema akiwasilisha taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Tabora (TUWASA) Mhandisi Mayunga Kashilimu amesema kukamilika kwa mradi huo kumewezesha wananchi zaidi ya milioni moja na laki mbili (1,200,000) wanapata huduma ya maji safi na salama.
“upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka hadi kufikia asilimia 100 katika Manispaa ya Tabora na miji ya Igunga, Nzega, Makao makuu ya Wilaya ya uyui pamoja na vijiji 102
Alisema huduma bora ya Maji inachangia kuboresha afya za wananchi wa maeneo husika na kuinua uchumi kupitia maendeleo ya sekta zingine zinazotegemea maji kama vile viwanda.
Kamati ya PAC, kesho inatarajia kukagua mradi wa kiwanda cha kupaka rangi mabomba kwa ajili ya kuweka mfumo wa upashaji joto mabomba katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga
Mwisho