WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, January 18, 2017

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YATEMBELEA SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) Bi. Nasama Massinda akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti walipotembelea Soko la Hisa leo Jijini Dar es Salaam.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bajeti walipotembelea Soko hilo leo Jijini Dar es Salaam

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa akifafanua jambo mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Bajeti walipotembelea Soko hilo leo Jijini Dar es Salaam

Meneja Miradi na Biashara wa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Patrick  akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi Soko hilo linavyofanya kazi.

Meneja Miradi na Biashara wa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Patrick  akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi Soko hilo linavyofanya kazi.

Meneja Miradi na Biashara wa wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Patrick  akiwaelezea Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi Soko hilo linavyofanya kazi.


KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA TAASISI YA UTAFITI WA MISITU

Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia wadudu wanaoshambulia misitu wakati walipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI) iliyoko Mkoa wa Morogoro.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Magembe akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusiana na kifaa maalumu ambacho kinawezesha kutambua kama kuna moto kwenye msitu. Wajumbe hao jana walitembelea Taasisi ya Utafiti wa Misitu (TAFORI) iliyoko Mkoa wa Morogoro.

Tuesday, January 17, 2017

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII WAANZA ZIARA MKOANI MOROGORO

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii walipotembelea Ofisi za Wakala wa Mbegu Nchini (TTSA) leo Mjini Morogoro

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii, Mhe. Atashista Nditiye akisikiliza maelezo kutoka kwa Mbaolojia wa Mbegu, kutoka Wakala wa Mbegu za Miti Nchini (TTSA), Ndugu Fandey Mashimba ya jinsi ya uoteshaji wa mbegu za miti
Mbaolojia wa Mbegu, kutoka Wakala wa Mbegu za Miti Nchini (TTSA), Ndugu Fandey Mashimba akiwalezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii namna ambavyo Wakala huo unavyozalisha mbegu za miti

Tuesday, December 13, 2016

SPIKA NDUGAI AKUTANA NA SPIKA BUNGE WA BUNGE LA ISRAEL

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Israel (Knesset) Mhe Yuli Yole Edelsten wakati Mhe Spika alipomtembelea Bungeni hapo. Mhe Ndugai yupo nchini Israel kwa ibada ya Hija.

Wednesday, December 7, 2016

SPIKA NDUGAI AAHIDI KUDUMISHA USHIRIKIANO NA CPA-AFRIKA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akizungumza na baadhi ya Wajumbe wa  wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika(CPA-AFRICA) jijini Dar es Salaam.Wakwanza kushoto ni Dkt. Acho Ihim Rais CPA-Afrika, Mhe Elijah Okupa Kaimu Mwekahazina wa CPA-Afrika na Mhe. Lindiwe Maseko Mwenyekiti wa kamati hiyo. Kamati hiyo ilikutana Jijini Dar es Salaam kwa muda wa wiki moja kujadili masuala mbalimbali yanayohusina na Chama hicho.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika jijini Dar es Salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati waliokaa) katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika (waliokaa) pamoja na Sekretarieti ya Chama hicho.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akiagana na Rais CPA-Afrika Dkt. Acho Ihim mara baada ya kufunga mkutano wa Chama hicho Jijini Dar es Salaam.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai ameahidi kudumisha ushirikiano na Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola-Kanda ya Afrika.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya chama hicho Mhe Ndugai amesema amekuwa Kiongozi na ameshiriki kwa muda mrefu katika shughuli za chama hicho na hivyo anaelewa mchango wa chama hicho katika kusaidia kusukuma mbele ajenda za Bara la Afrika katika Jumuiya ya Madola.
“Nipo pamoja nanyi na nimefanya kazi pamoja na Vingozi wengine katika Chama hiki katika kuzipeleka mbele ajenda za Bara la Afrika katika Jumuiya ya Madola,” alisema Mhe Ndugai.
Spika Ndugai aliongeza kuwa kwa kadri ambavyo Wabunge wapya wamekuwa wakichaguliwa ni vyema Wabunge wao wakaendelea kuelimishwa juu ya umuhimu wa Vyama vya Kibunge ikiwemo Chama cha Wabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola ili waweze kusaidia katika kusukuma mbele ajenda za bara la Afrika katika Vyama hivyo.
“Ninawahakikishia pia ushiriki wa Wabunge kutoka Bunge la Tanzania katika shughuli mbalimbali za chama hichi ikwemo Mkutano ujao wa 62 wa Chama cha Wabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola,” alisema Spika Ndugai.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati Tendaji wa CPA-Afrika Mhe Lindiwe Maseko alimshukuru Mhe Ndugai kwa ushirikiano ambao Bunge la Tanzania limeendelea kuonesha katika shughuli mbalimbali za CPA.
“Tunashukuru kwamba Tanzania imeendelea kuwa mwanachama hai wa CPA-Kanda ya Afrika na nimatumaini yetu kuwa mtaendelea kudumisha moyo huo,” alisema Mhe Maseko.