WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, September 6, 2022

NAIBU SPIKA ZUNGU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE LA WAWAKILISHI LA UFALME WA MOROCCO JIJINI RABAT.





Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Ufalme wa Morocco, Mhe. Rachid Talbi Alami katika kikao kilichofanyika leo tarehe 6 Septemba, 2022 katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Rabat Nchini Morocco.

Mazungumzo hayo yalijikita kuimarisha Uhusiano wa Kibunge baina ya Mabunge ya nchi hizo pamoja na kuimarisha Ushirikiano wa kiuchumi ikiwemo kilimo.

Mhe. Spika yupo nchini Morocco kwa zaiara ya kikazi ya siku 5.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akimpatia zawadi Spika wa Bunge la Wawakilishi la Ufalme wa Morocco, Mhe. Rachid Talbi Alami alipomtembelea leo tarehe 6 Septemba, 2022 Ofisini kwake Jijini Rabat Nchini Morocco.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiagana na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Ufalme wa Morocco, Mhe. Rachid Talbi Alami baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 6 Septemba, 2022 katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Rabat Nchini Morocco.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiongozana na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Ufalme wa Morocco, Mhe. Rachid Talbi Alami baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 6 Septemba, 2022 katika Ofisi za Bunge hilo Jijini Rabat Nchini Morocco.






 

Friday, September 2, 2022

WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI WAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA WIZARA YA NISHATI

 

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere (JNPP) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 2 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato akijibu hoja Mbalimbali za Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere (JNPP) kilichofanyika leo tarehe 2 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Mohamed Said Issa akichangia jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere (JNPP) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 2 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Ndg. Maharage Chande akijibu hoja Mbalimbali za Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere (JNPP) kilichofanyika leo tarehe 2 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.



Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere (JNPP) kilichofanyika leo tarehe 2 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO WAKABIDHI HOJA ZA MAPENDEKEZO YA KAMATI KWA SERIKALI (OFISI YA WAZIRI MKUU; SERA, BUNGE NA URATIBU)


Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichokabidhi hoja za Mapendekezo ya kamati kwa Serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu) zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene (katikati) akizungumza mbele ya Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakati wa kupokea hoja za kamati hiyo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022, kushoto kwake ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga



Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akichangia jambo wakati kamati hiyo ilipokabidhi hoja za Mapendekezo ya kamati kwa Serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu) zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022, Kushoto ni Mjumbe wa kamati hiyo, Mhe. Medard Kalemani


Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiwa katika kikao cha kukabidhi hoja za Mapendekezo ya kamati kwa Serikali (Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu) zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akipokea taarifa ya Mapendekezo ya kamati zilizowasilishwa katika Mkutano wa Saba wa Bunge ili ziweze kupatiwa majibu kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan tukio lililofanyika katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma leo tarehe 2 Septemba, 2022, Kulia ni katibu wa kamati hiyo, Ndg. Mkuta Masoli 

Saturday, August 27, 2022

NAIBU SPIKA ZUNGU AFUNGUA MAFUNZO YA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA KAMATI ZA USIMAMIZI ZA BUNGE (PAC, LAAC NA PIC) PAMOJA NA KAMATI YA BAJETI.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU Institute of Public Accountability, Ndg. Ludovick Utouh kabla ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.




Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akifungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mtendaji wa WAJIBU Institute of Public Accountability, Ndg. Ludovick Utouh akitoa neno la ukaribisho wakati wa mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa kamati za usimamizi wa Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti wakishiriki mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati hizo yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) baada ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.



Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) baada ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) baada ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.


Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa kamati ya Bajeti baada ya kufungua mafunzo ya uwazi na uwajibikaji kwa kamati za usimamizi za Bunge (PAC, LAAC na PIC) pamoja na kamati ya Bajeti yaliyofanyika leo tarehe 27 Agosti, 2022 katika hoteli ya Royal Village Jijini Dodoma.

 

Friday, August 5, 2022

MAAFISA WABUNGE WAENDELEA NA UTOAJI WA ELIMU KWA UMMA KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE KANDA YA KATI JIJINI DODOMA





 Maafisa Wabunge wakiendelea na utoaji wa elimu kwa umma kwa wageni mbalimbali wanaotembelea Banda la Bunge katika Maonyesho ya Nane Nane Kanda ya Kati leo Agosti 05, 2022 Nzuguni Jijini Dodoma.

Friday, July 15, 2022

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI POLEPOLE JIJINI LILONGWE


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi.




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (kushoto) alipomtembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe. Wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioambatana na Mhe. Spika


Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole akiwasilisha taarifa ya Mahusiano baina ya Tanzania na Malawi mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) katika ofisi za Ubalozi huo Jijini Lilongwe nchini Malawi. Wengine ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania walioambatana na Mhe. Spika



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipokea taarifa ya Mahusiano baina ya Tanzania na Malawi kutoka kwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole alipomtembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole alipotembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe.

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole (kulia kwake) alipotembelea Ubalozini hapo Jijini Lilongwe. Kuanzia kushoto ni Wabunge wa Bunge la Tanzania walioambatana na Mhe. Spika ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Kassim Haji, Mhe. Shally Raymond na Mhe. Dkt. Alfred Kimea.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ubalozini hapo Jijini Lilongwe.




SPIKA DKT. TULIA ATEMBELEA BUNGE LA MALAWI










 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson aungana na Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kutembelea Bunge la Malawi lililopo Jijini Lilongwe.