WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, August 28, 2023

SPIKA DKT. TULIA AMEONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JIJINI DODOMA









 

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Kumi na Mbili (12) wa Bunge leo tarehe 28 Agosti, 2023 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc

Mkutano huu wa wiki mbili utaanza kesho tarehe 29 Agosti, 2023 na unategemewa kuhitimishwa tarehe 8 Septemba, 2023.

Friday, August 18, 2023

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA, KILIMO NA MIFUGO YAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA.




Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. David Kihenzile akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Utendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Utendaji wa Bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala (wrrb) jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, Mhe. Kunti Majala akijadili taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Utendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Utendaji wa Bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala (wrrb) jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakati wa kujadili taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Utendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Utendaji wa Bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala (wrrb) jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe


Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakijadili taarifa ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Utendaji wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na Utendaji wa Bodi ya usimamizi wa stakabadhi za ghala (wrrb) jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.

 

 

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA YA WIZARA YA NISHATI




Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichopokea na kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mkurugenzi Mkuu wa wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy akiwasilisha taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili mbele ya Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.


Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Iddi Kassim Iddi akijadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.



Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato

Mwenyekiti wa Bodi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Ndg. Janeth Mbene akitolea maelezo hoja za Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati wa kujadili taarifa ya Wizara ya Nishati kuhusu hali ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya tatu, mzunguko wa pili jana tarehe 17 Agosti, 2023 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kulia ni Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Stephen Byabato na Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Iddi Kassim Iddi.


 

Wednesday, August 2, 2023

WATUMISHI WA OFISI YA BUNGE WAENDELEA NA UTOAJI WA ELIMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZILIZOPO ILALA JIJINI DAR ES SALAAM.













 Watumishi wa Ofisi ya Bunge wameendelea na utoaji wa elimu kuhusu Shughuli zinazofanywa na Bunge kwa wanafunzi wa Shule ya msingi ya Upanga, Shule ya msingi Kisutu na Shule ya Sekondari ya wasichana Kisutu leo tarehe 2 Agosti, 2023 Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ziara ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ilala.

Ziara hii imeanza tarehe 31 Julai, 2023 na inategemewa kuhitimishwa tarehe 11 Agosti, 2023.

Tuesday, August 1, 2023

WATUMISHI WA BUNGE WAENDELEA KUTOA ELIMU YA BUNGE MKOA WA LINDI






 

WATUMISHI OFISI YA BUNGE WATOA ELIMU KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZILIZOPO ILALA JIJINI DAR ES SALAAM















 Watumishi wa Ofisi ya Bunge wametembelea ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, watoa elimu kuhusu Shughuli zinazofanywa na Bunge kwa wanafunzi wa Shule za msingi za Bunge, Mtendeni na Msimbazi jana tarehe 31 Julai, 2023 Jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ziara ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ilala.

Ziara hii imeanza jana tarehe 31 Julai, 2023 na inategemewa kuhitimishwa tarehe 11 Agosti, 2023.