WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, July 27, 2017

SPIKA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA MASPIKA NA VIONGOZI WA UMOJA WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA



MHE. SPIKA APONGEZWA KWA USHINDI KATIKA MKUTANO WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA BARANI AFRIKA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akipongezwa na Naibu Spika wa Cameroon, Mhe.  Monjowa Lifaka baada ya kushinda nafasi ya Mwenyekiti  wa Maspika na Viongozi wa Bunge katika Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika. Uchaguzi huo umefanyika katika Mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika uliomalizika leo Mjini Abuja.

MHE. SPIKA AKIWA NCHINI NIGERIA KUHUDHURIA MKUTANO WA MASPIKA



 Mhe. Spika Job  Ndugai akiwa katika mazungumzo na Maspika wa Nchi za Uganda (kwanza kushoto) Mhe. Rebeka Kadaga ,Afrika Kusini (pili kushoto)Mhe. Thandi Modise na Naibu Spika wa Cameroon kulia) Mhe. Monjowa Lifaka .Spika Ndugai yuko nchini Nigeria kuhudhuria mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika.


 Mhe. Spika Job  Ndugai akiwa katika mazungumzo na Maspika wa Nchi za Uganda (kwanza kushoto) Mhe. Rebeka Kadaga ,Afrika Kusini (pili kushoto)Mhe. Thandi Modise na Naibu Spika wa Cameroon kulia) Mhe. Monjowa Lifaka .Spika Ndugai yuko nchini Nigeria kuhudhuria mkutano wa Maspika wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Barani Afrika.


Wednesday, July 19, 2017

MHESHIMIWA SPIKA AHUDHURIA MAZISHI YA MKE WA DKT. HARRISON MWAKYEMBE

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha Maombolezo wakati wa mazishi ya Mke wa Waziri Wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Dkt Harrison Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimfariji Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati mazishi ya Mke wake, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimsabai Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati mazishi ya Mke wake, Marehemu Linah Mwakyembe Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.

 Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akitoa Salamu za Heshima kwa mwili wa Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa mazishi yake nyumbani kwake Wilayani Kyela, Jijini Mbeya.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa kwanza toka kushoto)Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai, Naibu Spika Dkt Tulia Ackson wakifuatilia misa ya mazishi ya Mke wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa mazishi yake nyumbani kwake Wilayani Kyela, Jijini Mbeya

SPIKA APATA UGENI KUTOKA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA WA HAKI ZA BINADAMU

Spika wa Bunge,  Mhe.  Job Ndugai (kulia) akimueleza jambo Mtaalamu wa kujitegemea kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, lipo Geneva, Switzerland Ndg. Ikponwosa Ero,  nyumbani kwake Mjini Dodoma. katikati ni Katibu wa Spika, Ndg. Said Yakubu. 



Spika akiwa na ugeni  huo kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu lenye Makao Makuu yake Geneva, Switzerland wakiongozwa na Ndg. Ikponwosa Ero (wa pili kushoto) uliomtembelea nyumbani kwake Mjini Dodoma.


Add caption
Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimsikiliza Mtaalamu wa kujitegemea kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Ndg. Ikponwosa Ero ,  nyumbani kwake Mjini Dodoma. katikati ni katibu wa Spika, Ndg. Said Yakub

Thursday, July 13, 2017

SPIKA ATEMBELEWA NA RAIS MSTAAFU WA IRELAND NA MAMA GRACA MACHEL

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto)akisalimiana na Rais Mstaafu wa Ireland (kulia) Mheshimiwa Mary Robnson ambae pia ni Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya. Katikati ni Mama Graca Machel .Tukio lilimefanyika leo katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma baada ya wageni hao kutembelea Bunge.

Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza na wageni kutoka  Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya  "The Elders"  walipomtembelea leo ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland  Mheshimiwa Mary Robinson ni Mama Graca Machel


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akimkabidhi  Picha ya Jengo la Bunge la Tanzania Rais Mstaafu wa Ireland Mheshimiwa Mary Robinson wakati  alipotembelea Ukumbi wa Bunge la Tanzania ulipo Mjini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Mjumbe wa  “The Elders” Taasisi inayoshughulika na Amani, Haki za Binadamu na Huduma za Afya, Mama Graca Machel (kushoto) katika kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, katikati ni Rais Mstaafu wa Ireland ambae pia ni Mjumbe kutoka Taasisi hiyo Mheshimiwa Mary Robinson
Rais Mstaafu wa Ireland, Mheshimiwa Mary Robinson akitoa neno la shukrani kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai mara baada ya  kutembelea Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma kulia ni Mama Graca Machel