WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 26, 2018

KAMATI YA PAC YATEMBELEA MIRADI INAYOTEKELEZWA NA VETA MWANZA NA MRADI WA UJENZI WA ROCKY CITY MALL

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo , Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndugu John Mongela wakitoka ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo kabla ya kuanza  ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa katika Jiji hilo.

 Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) wakionyeshwa baadhi ya vifaa  vilivyonunuliwa kwa  ajili ya Karakana inayoendekea kujengwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akiongozana na uongozi wa Mamlaka ya Ufundi Stadi  VETA kwenda kukagua mradi wa ujenzi wa Karakana unaotekelezwa na Mamlaka hiyo

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakielekea kukagua Mradi ya ujenzi wa Karakana unaotekelezwa na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi VETA Mkoa wa Mwanza.

Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akitoa maelekezo kwa uongozi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mwanza baada ya Kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa Karakana.

Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)  wakiwasili katika Jengo la Rocky City Mall lililopo Jijini Mwanza kwa ajili ya kukagua mradi huo uliotekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na Mfuko wa Pensheni wa LAPF. Mbele ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka na Mkurugenzi Mkuu wa LAPF Ndugu Eliudi Sanga.

Wajumbe wa Kamati ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakionyeshwa baadhi ya maeneo ndani ya Jengo la Rocky City Mall. Pichani wakiangalia chumba ambacho kinadhibiti hali ya usalama katika maeneo yote ya jengo hilo


Wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)  wakiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF na Halmashauri ya Jiji la Mwanza kujadili utekelezaji wa mradi wa Jengo la  Rocky City Mall  unaotekelezwa kwa ubia kati ya Halmashauri ya Jiji hilo na LAPF. 


Friday, March 23, 2018

WAJUMBE WA KAMATI YA LAAC NA PAC WAKIWA KATIKA SEMINA YA KUJENGEWA UWEZO MKOA WA SINGIDA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada ya jinsi ya kujenga mtandao (Networking) kutoka kwa Mkaguzi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Rweyimamu katika semina inayofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada ya jinsi ya kujenga mtandao (Networking) kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Rweyimamu katika semina inayofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza katika semina ya wajumbe wa Kamati hiyo na wajumbe Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), semina inayofanyika Mkoani Singida imeandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NOAT) kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC MheshimiwaVedasto Ngombale na kulia ni Ndugu Rweyimamu  kutoka  NOAT

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mheshimiwa Naghenjwa Kaboyoka akizungumza katika semina ya wajumbe wa Kamati hiyo na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), semina inayofanyika Mkoani Singida imeandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao.


Thursday, March 22, 2018

WAJUMBE WA KAMATI YA LAAC NA PAC WAENDELEA NA MAFUNZO MKOANI SINGIDA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada kuhusu  Mtazamo wa kikaguzi kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Athuman Mbuttuka katika semina iliyofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada kuhusu  Mtazamo wa kikaguzi kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Athuman Mbuttuka katika semina iliyofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Mary Chatanda akichangia hoja katika  semina ya kuwajengea uwezo wajumbe wa Kamati hiyo, iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kufanyika Mkoa wa Singida.

NAIBU SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS WA BUNGE LA VIETNAM PAMOJA NA UJUMBE WAKE JIJINI DAR ES SALAAM.



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson akizungumza na Ujumbe wa Wabunge toka Bunge la Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam ukiogozwa na Makamu wa Rais wa Bunge hilo Mhe. Phung Ouoc Hien. Mazungumzo hayo yamefanyika mapema leo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam wakati Wabunge hao walipofanya ziara ya Kibunge yenye lengo lakukuza uhusiano baina ya pande zote mbili.



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson wa (kwanza kushoto) akizungumza na Ujumbe wa Wabunge toka Bunge la Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam ukiogozwa na Makamu wa Rais wa Bunge hilo Mhe. Phung Ouoc Hien (wa nne toka  kulia).



Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson akipokea zawadi toka kwa Makamu wa Rais wa Bunge la Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mhe. Phung Ouoc Hien mara baada ya mazungumzo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson (wa sita toka kulia) katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Wabunge toka Bunge la Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam ukiogozwa na Makamu wa Rais wa Bunge hilo Mhe. Phung Ouoc Hien  (wa kwanza kulia kwa Naibu Spika) mara baada ya mazungumzo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

Wednesday, March 21, 2018

WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA LAAC NA PAC WAENDELEA NA MAFUNZO YA KUJENGEWA UWEZO KATIKA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI MKOANI SINGIDA

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada kuhusu  ukaguzi wa ufanisi kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Jmaes Pilly katika semina iliyofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC),wakifuatilia mada kuhusu  ukaguzi wa ufanisi kutoka kwa Mkaguzi wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Ndugu Jmaes Pilly katika semina iliyofanyika Mkoani Singida kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajumbe hao.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), wakiwa katika picha ya pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa Mussa Assad.

 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Profesa  Mussa Assad akisisitiza jambo katika semina kwa  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyofanyika Mkoani Singida ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao.