WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 31, 2022

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI BUNGENI JIJINI DODOMA




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi cha kupokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Tisa wa Bunge leo tarehe 31 Oktoba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa mwihambi, ndc akishiriki katika kikao cha kamati ya uongozi cha kupokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Tisa wa Bunge leo tarehe 31 Oktoba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Emmanuel Mwakilasa


 

Wajumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge wakiwa katika kikao cha kamati hiyo cha kupokea na kujadili Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano wa Tisa wa Bunge leo tarehe 31 Oktoba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya katibu na Sheria, Mhe. Joseph Mhagama na Makamu Mwenyekiti wa Hesabu za Serikali, Mhe. Japhet Hassunga.

 

Friday, October 21, 2022

WAJUMBE CWP KANDA YA AFRIKA WAENDELEA NA WARSHA YA UHAMASISHAJI KUHUSU WABUNGE WANAWAKE KATIKA UONGOZI NA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM



Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region) na Duniani, Mhe. Dkt. Zainab Gimba akiongoza majadiliano katika warsha ya uhamasishaji kwa Wajumbe wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyoanza jana inategemea kumalizika leo uku ikiwa imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.



Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Ruth Meena akitoa mada kuhusu migogoro Mbalimbali wanayokutana nayo Wabunge wanawake baada ya uchaguzi katika warsha ya uhamasishaji kwa Wajumbe wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region) kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyoanza jana inategemea kumalizika leo uku ikiwa imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.




Wajumbe wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region) wakimsikiliza Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Ruth Meena (hayupo kwenye picha) akitoa mada kuhusu migogoro Mbalimbali wanayokutana nayo Wabunge wanawake baada ya uchaguzi katika warsha ya uhamasishaji kwa Wajumbe hao kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyoanza jana inategemea kumalizika leo uku ikiwa imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.



 Mjumbe wa kamati ya uongozi ya Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CWP Africa Region), Mhe. Ndangiza Madina akichangia jambo wakati wa warsha ya uhamasishaji kwa Wajumbe wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyoanza jana inategemea kumalizika leo uku ikiwa imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.

Thursday, October 20, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFUNGUA WARSHA YA UHAMASISHAJI CHAMA CHA WANAWAKE WA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA






Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua warsha ya uhamasishaji kwa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika leo tarehe 20 Oktoba, 2022 katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo inategemea kufanyika kwa muda wa siku mbili na imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.



Mwenyekiti wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Mhe. Dkt. Zainab Gimba akizungumza katika warsha ya uhamasishaji kwa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika leo tarehe 20 Oktoba, 2022 katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo inategemea kufanyika kwa muda wa siku mbili na imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.



Katibu wa Bunge ambaye pia ni Katibu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika, Ndg. Nenelwa Mwihambi, ndc akizungumza katika warsha ya uhamasishaji kwa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika leo tarehe 20 Oktoba, 2022 katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo inategemea kufanyika kwa muda wa siku mbili na imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.





Wajumbe wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika wakishiriki katika warsha ya uhamasishaji ya Chama hicho kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika leo tarehe 20 Oktoba, 2022 katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo inategemea kufanyika kwa muda wa siku mbili na imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.



 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Chama cha Wanawake wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika baada ya kufungua warsha ya uhamasishaji ya Chama hicho kuhusu Wabunge Wanawake katika uongozi na siasa iliyofanyika leo tarehe 20 Oktoba, 2022 katika hoteli ya Ramada Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhe. Dkt. Zainab Gimba

Warsha hiyo inategemea kufanyika kwa muda wa siku mbili na imehudhuriwa na nchi 10 za Afrika.

Wednesday, October 19, 2022

WADAU WATOA MAONI KUHUSU MISWADA MINNE YA SHERIA

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo akitoa maoni yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Jamii Forums Tanzania Ndg. Maxence Melo  akiwasilisha maoni ya Taasisi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakipokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 3 wa Mwaka 2022.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakijadili maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022.

Wadau mbalimbali wakishiriki kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote wa Mwaka 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo.
Mwakilishi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania Ndg. Paul Kisabo akiwasilisha maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo.
 

Wednesday, October 12, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA SPIKA WA BUNGE LA KOREA KUSINI, SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA JAMHURI YA INDONESIA NCHINI RWANDA




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Spika wa Bunge la Korea Kusini, Mhe. Jin Pyo Kim katika ofisi ndogo za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini humo.

Mhe. Spika ameambatana na Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wawakilishi katika Umoja huo.



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge Spika wa Bunge la Korea Kusini, Mhe. Jin Pyo Kim tukio lililofanyika katika ofisi ndogo za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini humo.



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiagana na Spika wa Bunge la Korea Kusini, Mhe. Jin Pyo Kim baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) Nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini humo.



Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Indonesia, Mhe. Dkt. Puan Maharani walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kigali (KCC) nchini Rwanda leo tarehe 12 Oktoba, 2022 wakati wa Mkutano wa 145 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea nchini humo.

 

Monday, October 3, 2022

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AMUAPISHA MBUNGE MTEULE MHE. ANGELLAH KAIRUKI JIJINI DAR-ES-SALAAM

Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiapa katika ofisi ndogo ya Bunge Jijini Dar-es-salaam.

Spikawa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akishuhudia Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiweka saini mara baada ya kuapishwa katika ofisi ndogo ya Bunge Jijini Dar-es-salaam.



 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Tulia Ackson (Mb) amuapisha Mhe. Angellah Kairuki (Mb) aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais Mhe. Samia S. Hassan jana tarehe 02 Oktoba 2022