WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, March 7, 2019

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA OFISI ZA TRA ARUSHA

 Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, wakiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Mkoa wa Arusha wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo na kupatiwa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusiana na jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki  (ETS) unavyofanya kazi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti,Mhe George Simbachawene akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Kamati yake na uongozi wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA)  Mkoa wa Arusha wakati Kamati hiyo ilipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo na kupatiwa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusiana na jinsi Mfumo wa Stempu za Kielektroniki  (ETS) unavyofanya kazi

Wednesday, March 6, 2019

KAMATI YA BAJETI YAFANYA KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao kati ya Kamati hiyo na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Kamati ilitembelea Halmashauri hiyo kwa lengo la kuangalia  utekelezaji wa Mfumo Akaunti Jumuifu (TSA).

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao kati ya Kamati hiyo na uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,kulia kwake ni Kaimu Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Ali Banange na kushoto kwake ni Katibu wa Kamati hiyo Ndugu Michael Kadebe. Kamati ilitembelea Halmashauri hiyo kwa lengo la kuangalia  utekelezaji wa Mfumo Akaunti Jumuifu (TSA).

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia mfumo wa Akaunti Jumuifu (TSA) katika Halmashauri ya Jiji la Arusha jinsi unavyofanya kazi. Kamati ilitembelea Halmashauri hiyo kwa lengo la kuangalia  utekelezaji wa Mfumo Akaunti Jumuifu (TSA).

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WATEMBELEA BENKI KUU ARUSHA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Naibu Gavana Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dkt. Yamungu Kayandabila wakati kamati hiyo ilipotembelea Benki hiyo Kanda ya Arusha.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene wakiwa katika kikao cha pamoja na uogozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati Kamati ilipotembelela benki hiyo Kanda ya Arusha kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Mfumo Akaunti Jumuifu (TSA).

Naibu Gavana Uchumi na Sera wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt. Yamungu Kayandabila,akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Bajeti katika kikao cha pamoja. Kamati ya Bajeti ilitembelea Banki Kuu Kanda ya Arusha  kwa ajili kuangalia utekelezaji wa Mfumo Akaunti Jumuifu (TSA). pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. George Simbachawene.


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene wakiwa katika kikao cha pamoja na uogozi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati Kamati ilipotembelela benki hiyo Kanda ya Arusha kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa Mfumo Akaunti Jumuifu (TSA).

Tuesday, March 5, 2019

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGENEZA TRANSFOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akiwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) , Ndugu Zahir Salim wakati Kamati ilipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) kilichopo Arusha , pembeni ya Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ndugu Zahir Salim.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) , Ndugu Zahir Salim akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi mitambo mbalimbali ya kuzalisha transfoma inavyofanya kazi, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani. Kamati ilitembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC) , Ndugu Zahir Salim akiwaelezea wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti jinsi mitambo mbalimbali ya kuzalisha transfoma inavyofanya kazi, pembeni yake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani. Kamati ilitembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha

Mfanyakazi wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANALEC), Sara Laizer akielezea majukumu yake kwa wajumbe kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Kamati hiyo ilitembelea kiwanda hicho kilichopo Arusha. Nyuma yake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakitembelea Kiwanda cha kutengeneza Transfoma (TANELEC kuona jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi, wa kwanza mbele ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. George Simbachawene, Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ndugu Zahir Salim na Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani. Kamati ilitembelea Kiwanda hicho kilichopo Jijini Arusha

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Mhe. George Simbachawene akipanda mti wa kumbukumbu wakati Kamati hiyo ilipotembelea Kiwanda cha Kutengeneza Tansfoma TANALEC kilichopo Arusha. Nyuma ni Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Daqarro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho, Ndugu Zahir Salim

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani na uongozi wa Kiwanda cha kutengeneza Transfoma  cha TANELEC, wajumbe hao walitembelea Kamati hiy kuona jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi.

Monday, March 4, 2019

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiwa wameambatana na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakitembelea maeneo mbalimbali ya chuo hicho katika ziara ya Kamati.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiwa katika kikao cha pamoja na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha (AIA) wakati Kamati hiyo ilipotembelea chuo hicho.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti , Mhe. George Simbachawene akizungumza katika kikao cha Kamati hiyo na uongozi wa Chuo cha Uhasibu Arusha  (AIA) wakati Kamati hiyo ilipotembelea chuo hicho.kushoto kwake ni Naibu Mkuu wa Baraza la Chuo hicho,  Ndugu Juma Kaniki na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo.

KAMATI YA BAJETI YATEMBELEA KIWANDA CHA GENERAL TYRE ARUSHA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakitembelea kiwanda cha General Tyre kilichoko Arusha. Wajumbe hao wapo katika ziara ya siku saba Mkoani Arusha.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. George Simbachawene wakiangalia mitambo iliyotumika kutengeneza matairi katika kiwanda cha General Tyre kilichoko Arusha, mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo (NDC), Profesa Damian Gabagambi. Wajumbe hao wapo katika ziara ya siku tano Mkoani Arusha

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WAANZA ZIARA MKOANI ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti ofisini kwake wakati Kamati hiyo ilipomtembelea kabla ya kuanza ziara yake katika Mkoa huo.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo wakati Kamati hiyo ilipomtembelea ofisini kwake kabla ya kuanza ziara yake katika Mkoa huo.