WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Thursday, August 29, 2019

SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AKAGUA MAANDALIZI YA MKUTANO WA CPA



Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali Maulid amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa waliyoipata ya kuwa wenyeji wa  Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kujitangaza kibiashara na kitalii.

Mheshimiwa Maulid ametoa rai hiyo leo Kisiwani Zanzibar wakati akikagua maandalizi ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Agosti hadi septemba 5 mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business & Spa.

Alisema mkutano huo kufanyika Zanzibar utafungua fursa katika sekta za biashara ikiwemo utalii na kuwataka Watanzania kuonyesha ukarimu kwa wageni hao.

“Tuonyeshe ukarimu wakati kupokea wageni hawa, tuitendee haki nchi yetu, tukikaa nao vizuri wageni wetu itatosha kwa sisi kujitangaza, tutumie fursa hii kwa kadri tutakavyoona inaweza kuisaidia nchi” alisema.

Alisema mkutano huo ni wa kihistoria kwa kuwa unaweza kuvunja rekodi ya mahudhurio ya wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchi 18 wanachama ambao unajumuisha maspika, manaibu spika na wabunge.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPA, Tawi la Zanzibar, Mheshimiwa Simai Mohammed Said alisema mkutano huo mbali na kutoa fursa za kiuchumi lakini pia utawezesha wajumbe kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuisimamia Serikali katika mambo yanayogusa wananchi.

Awali akizungumzia maandalizi ya awali, Katibu Msaidizi wa CPA, Kanda ya Afrika, Said Yakubu alisema Nchi zote 18 wanachama zimethibitisha ushiriki na kwamba maspika 23 kutoka mabunge makubwa na madogo watahudhuria.

Alisema nchi wanachama wa CPA, Kanda ya Afrika ni Botswana, Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Siera – Leone, Afrika ya Kusini, Tanzania, Uganda na Zambia.



SPIKA WA BUNGE MHESHIMIWA JOB NDUGAI AKARIBISHA USHIRIKIANO NA NCHI YA IRELAND

Spika wa Bunge Mheshimiwa, Job Ndugai ameishukuru Serikali ya Ireland kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya sheria na haki za binadamu.
Mheshimiwa Spika ametoa shukrani hizo leo ofisini kwake Bungeni JIjini Dodoma wakati alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria wa haki za binadamu kutoka Ubalozi wa Ireland wakiongozwa na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini Mheshimiwa Bronagh Carr.
Alisema Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano huo na Serikali ya Ireland katika masuala hayo ya sheria pamoja na kudumisha haki za binadamu.
Aidha, alisema upo umuhimu ujumbe huo, ukakutana na Umoja wa Wabunge Wanawake nchini (TWPG) ili kujadili changamoto za kijinsia zilizopo katika maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi kwa kuwa Ireland imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya usawa wa kijinsia.
aliwataka pia wakutane na  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambapo miswada yote inayoathiri huduma za jamii ikiwemo masuala ya elimu na jinsia hujadiliwa kwenye kamati hiyo kabla ya kuingia Bungeni.
“Katika suala la usawa kwa jinsia Bunge letu limepiga hatua kubwa ambapo Wabunge wa Viti Maalum Wanawake ni asilimia 30 ya Wabunge wote 393 pia wapo Wabunge wa majimbo ambao ni Wanawake hivyo kuongeza nafasi ya uwakilishi wa jinsi hiyo Bungeni” alisema Mheshimwa Spika.
kwa upande wake Kaimu Balozi wa Ireland, Mheshimiwa Bronagh Carr alimshukuru Mheshimiwa Spika kwa kukubali kukutana nae pamoja na Kamati za Bunge.
Alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland umekuwepo kwa kipindi cha miaka 40 na unazidi kuimarika siku hadi siku.
Ujumbe huo umelenga kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya kisheria  ikiwemo Wabunge, Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali pamoja na Jeshi la polisi nchini ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya sheria na jinsia.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini walipokutana na kufanya mazungumzo Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo. 
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifafanua jambo alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini waliomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo.


Friday, August 23, 2019

KATIBU WA BUNGE ATEMBELEWA NA JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA DODOMA



Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akizungumza na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Lameck Mlacha wakati Jaji huyo alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jjijini  Dodoma.


Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Lameck Mlacha wakati Jaji huyo alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai akiagana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Lameck Mlacha mara baada ya Jaji huyo kumtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma.

Tuesday, August 20, 2019

WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WAKIWA KATIKA KIKAO

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma


Afisa Bajeti kutoka Ofisi ya Bunge, Maombi Kakozi akifafanua jambo  kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma

WAJUMBE WA KAMATI YA NISHATI WAPOKEA TAARIFA YA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MIRADI YA REA

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati, Mhe. Dunstun Kitandula akifuatilia jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo, Felister Mgonja.


Waziri wa Nishati, Mhe. Medard Kalemani akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati ambapo Wizara yake iliwasilisha Taarifa ya Maendeleo na Utekelezaji wa Miradi ya REA, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, pembeni yake ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo ambapo walipokea Taarifa ya Maendeleo na Utekelezaji wa Miradi ya REA kutoka Wizara ya Nishati, kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAJADILI MUSWADA WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO WA MWAKA 2019



Mshauri wa Masuala ya Sheria wa Bunge Ndg. Mosi Lukuvi

 akitoa maelezo ya uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Serikali 

Mtandao 2019  (The e-Gvernment Act 2019),kwa Kamati ya 

Utawala na Serikali za Mitaa,Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Nchemba na 

katikati ni Katibu wa Kamati hiyo Ndg. Chacha Nyakega. 

Mshauri wa Masuala ya Sheria wa Bunge Ndg. Mosi Lukuvi

 akitoa maelezo ya uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Serikali 

Mtandao 2019  (The e-Gvernment Act 2019),kwa Kamati ya 

Utawala na Serikali za Mitaa,Jijini Dodoma. Kulia ni Makamu 

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Mwanne Nchemba na 

katikati ni Katibu wa Kamati hiyo Ndg. Chacha Nyakega. 

Wajumbe wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa wakisikiliza

 maelezo ya uchambuzi wa Muswada wa Sheria ya Serikali 

Mtandao 2019  (The e-Gvernment Act 2019)kutoka kwa Mshauri 

wa Masuala ya Sheria wa Bunge Ndg. Mosi Lukuvi.