WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, November 10, 2020

MHE. NDUGAI ACHAGULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE LA 12



Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Y. Ndugai akijinadi wakati akigombea kuwa Spika wa Bunge la 12.

Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Y. Ndugai akiapa mara baada ya kuchaguliwa  kuwa Spika wa Bunge la 12.
Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Y. Ndugai akipokea vitendea kazi kutoka kwa Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai mara baada ya kuchaguliwa  kuwa Spika wa Bunge la 12.
Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Y. Ndugai akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kuchaguliwa  kuwa Spika wa Bunge la 12.

Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Y. Ndugai akizungumza mara baada ya kuchaguliwa  kuwa Spika wa Bunge la 12.

 

Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 12, umeanza kwa kumchagua Mbunge wa Kongwa, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai (Mb) kuwa Spika wa Bunge hilo kwa kura 344 kati ya kura 345 zilizopigwa ushindi ambao ni sawa na asilimia 99.7.


Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai katika kikao cha uchaguzi huo ambacho kiliongozwa na mwenyekiti wa muda, Mheshimiwa William Lukuvi.


Akizungumza mara baada ya kiapo, Mheshimiwa Ndugai aliwashukuru wabunge kwa ushindi huo wa kishindo huku akiwataka Wabunge wote hususani wale wapya kusoma Kanuni za kudumu za Bunge pamoja na Sheria mbalimbali zinazohusiana na Bunge.


"Muwe tayari kuchapa kazi kama kuna tatizo lolote msisite kuja kuniona bila wasiwasi wowote mimi nipo kwa ajili yenu wote,” alisema.


Aidha, alisema uwepo wa wabunge wengi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) haina maana kwamba Bunge hilo litakuwa Bunge la ‘Ndiyo Mzee’ na kuwataka wabunge hao wasisikilize maneno ya watu badala yake wachape kazi.


"Mimi nakataa kwamba kuwepo Wabunge wengi wa CCM humu ndani haimaanishi ndiyo kila kitu watu wataitikia ndiyo au hapana hapana utekelezaji wa majukumu utafanyika Kama kawaida.” alisema Mheshimiwa Ndugai.


“Hata hivyo mkiamua kuwa mabubu ili muonekane mna nidhamu shauri zenu kwani mtatoa majibu kwa wananchi waliowachagua muwasemee mambo yao baada ya miaka mitano,” alisema.


Mheshimiwa Ndugai aliwaambia Wabunge wa upinzani kwamba licha ya uchache wao Bungeni lakini wana haki zote kama Wabunge wengine hivyo na wao lazima wasikike.


Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa kwanza wa Bunge la Kumi na Mbili kimeendelea pia na uapisho kwa wabunge wateule.


Thursday, August 13, 2020

WATUMISHI WA KITENGO CHA TEHAMA WAPEWA MAFUNZO KUHUSU MFUMO WA KADI YA TATHIMINI NA UWAJIBIKAJI WA MALARIA



Watumishi wa Kitengo cha TEHAMA wa Ofisi ya Bunge wakipatiwa mafunzo kuhusu mfumo wa Kadi ya Tathimini na Uwajibikaji wa Malaria kutoka kwa Ndugu Khalifa Munisi. Mafunzo hayo yameandaliwa na Umoja wa Wabunge walio katika Mapambano dhidi ya Malaria (TAPAMA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia Programu ya Taifa ya Kupambana na Kutokomeza Malaria pamoja na Sekretarieti ya Maraisi na Viongozi wa Afrika walioungana kupambana na Malaria. Lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa kitengo hicho ili waweze kuiwasaidia wabunge kutumia Kadi hiyo kupitia kwenye vishikwambi (‘tablet’) vyao.

Mafunzo yakiendelea katika Ukumbi wa Msekwa B

Mafunzo yakiendelea


 

Tuesday, July 7, 2020

WANANCHI WENGI WAVUTIWA NA BANDA LA BUNGE MAONYESHO YA SABASABA

Afisa Mwandamizi wa Bunge Ndg. Louise Mdachi akitoa Elimu kwa wageni mbalimbali waliofika kutembelea Banda la Bunge kwenye Maonyesho ya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam hii leo. 

Afisa wa Bunge Ndg. Peter Magati akitoa Elimu kwa wageni mbalimbali waliofika kutembelea Banda la Bunge kwenye Maonyesho ya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam hii leo.

Afisa wa Bunge Ndg. Rehema Kipera akitoa Elimu kwa wageni mbalimbali waliofika kutembelea Banda la Bunge kwenye Maonyesho ya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam hii leo.

Sunday, July 5, 2020

WANANCHI MBALIMBALI WAENDELEA KUTEMBELEA BANDA LA BUNGE SABASABA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Damas Ndumbalo akisaini Kitabu cha Mahudhurio ya Wageni Mahsusi wanatembelea Banda la Bunge ili kupata Elimu kuhusiana Shughuli za Mhimili huu wa Kutunga Sheria. 

Afisa wa Bunge Ndg. Amina Salum akitoa ufafanuzi kwa Wageni mbalimbali wanaofika kwenye Banda la Bunge ili kupata Elimu kuhusiana Shughuli za Mhimili huu wa Kutunga Sheria. 

Afisa wa Bunge Ndg. Katherine Kaihula akitoa ufafanuzi kwa Wageni mbalimbali wanaofika kwenye Banda la Bunge ili kupata Elimu kuhusiana Shughuli za Mhimili huu wa Kutunga Sheria. 

Afisa wa Bunge Ndg. Zanele Chiza akifafanua jambo kwa Wageni mbalimbali wanaofika kwenye Banda la Bunge ili kupata Elimu kuhusiana Shughuli za Mhimili huu wa Kutunga Sheria.