WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Tuesday, January 21, 2020

KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA WIZARA YA MADINI

Waziri wa Madini , Mhe. Doto Biteko akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Wizara hiyo iliwasilisha taarifa ya upatinakaji wa fedha na utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha nusu mwaka  pamoja na taarifa ya kuhusu hatua zilizofikiwa katika uendelezaji wa leseni katika mradi wa Liganga na Mchuchuma.

Waziri wa Madini , Mhe. Doto Biteko akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Wizara hiyo iliwasilisha taarifa ya upatinakaji wa fedha na utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha nusu mwaka  pamoja na taarifa ya hatua zilizofikiwa katika uendelezaji wa leseni katika mradi wa Liganga na Mchuchuma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Simon Msanjila.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dustan Kitandula akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo lichofanyika Bungeni Jijini Dodoma. Kamati hiyo ilipokea taarifa ya Wizara ya Madini kuhusu upatinakaji wa fedha na utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha nusu mwaka pamoja na taarifa ya hatua zilizofikiwa katika uendelezaji wa leseni katika mradi wa Liganga na Mchuchuma. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo, Ndugu Felister Mgonja.


WIZARA YA AFYA YAKUTANA NA KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu akitoa taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara (Fungu 52) kwa kipindi cha nusu mwaka 2019/2020 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii hii leo Jijini Dodoma. 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mheshimiwa Salma Kikwete (katikati) akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara (Fungu 52) kwa kipindi cha nusu mwaka 2019/2020 hii leo Jijini Dodoma. 

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mheshimiwa Joseph Mbilinyi akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokutana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupokea taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Wizara (Fungu 52) kwa kipindi cha nusu mwaka 2019/2020 hii leo Jijini Dodoma. 



Friday, January 17, 2020

KAMATI YA PIC YAKUTANA NA UONGOZI WA BENKI YA NMB

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Dkt. Raphael Chegeni akizungumza katika kikao cha kamati Bungeni Jijini Dodoma.kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Benki ya NMB kwa ajili ya kupokea taarifa ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika Benki hiyo.


Wajumbe wa Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakiwa katika kikao cha kamati Bungeni Jijini Dodoma.kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Benki ya NMB kwa ajili ya kupokea taarifa ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika Benki hiyo.Pembeni yake ni Katibu wa Kamati, Elieka Saanya.

Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Profesa Joseph Semboja akizungumza katika kikao cha Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Benki hiyo kwa ajili ya kupokea taarifa ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika Benki hiyo.kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  Ndugu Ruth Zaipuna.

Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ndugu Ruth Zaipuna akizungumza katika kikao cha Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma.kamati hiyo ilikutana na uongozi wa Benki hiyo kwa ajili ya kupokea taarifa ya uwekezaji uliofanywa na Serikali katika Benki hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Profesa Joseph Semboja.


KAMATI YA NISHATI NA MADINI YAKUTANA NA TPDC

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa katika kikao cha kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, ambapo kamati ilipokea Taarifa ya utekelezaji na hali ya upatikanaji wa fedha za maendeleo katika Kampuni ya Taifa ya Mafuta (TPDC) kwa kipindi cha nusu mwaka.


Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akisikiliza kwa makini hoja za wabunge katika katika kikao cha kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, ambapo kamati ilipokea Taarifa ya utekelezaji na hali ya upatikanaji wa fedha za maendeleo katika Kampuni ya Taifa ya Mafuta (TPDC) kwa kipindi cha nusu mwaka.kulia ni Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Dkt. Adelardus Kilangi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dunstan Kitandula akisikiliza hoja za wajumbe katika kikao cha kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma, ambapo kamati ilipokea Taarifa ya utekelezaji na hali ya upatikanaji wa fedha za maendeleo katika Kampuni ya Taifa ya Mafuta (TPDC) kwa kipindi cha nusu mwaka.kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Felister 

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAKUTANA NA TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa. Kikao hicho cha Kamati kilifanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakiwa katika kikao cha Kamati Bungeni Jijini Dodoma ambapo walikutana na watendaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakiongozwa na Waziri Mhe. Selemani Jafo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Mwanne Nchemba akizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Bungeni Jijini Dodoma ambapo walikutana na na watendaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wakiongozwa na Waziri Mhe. Selemani Jafo.

Wednesday, January 15, 2020

MATUKIO MBALIMBALI WAKATI KAMATI YA PIC WAKIJADILI TAARIFA YA TAZARA



TANZIA


WAJUMBE WA KAMATI YA NISHATI WAJADILI TAARIFA YA REA

Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani akizungumza katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Nishati. Wizara hiyo iliwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji na hali ya upatikanaji wa fedha za Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini (REA).Pembeni yake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhe. Subura Mgalu. Kikao hicho cha kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati, Mhe. Dunstan Kitandula akizungumza katika kikao cha Kamati. Kamati hiyo ilipokea na kujadili taarifa kuhusu utekelezaji na hali ya upatikanaji wa fedha za Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini (REA).Pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo Felister Mgonja. Kikao hicho cha kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati wakiwa katika kikao cha kamati hiyo ambapo walikutana na watendaji wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Umeme Vijijni. Kikao hicho cha kamati kimefanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.