WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Friday, November 27, 2020

OFISI YA BUNGE YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI ZA BUNGE

Waandishi wa habari za Bunge wakifuatilia kwa makini mada zilizowasilishwa kwenye Mafunzo ya Waandishi hao yaliyofanyika kwenye hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka gazeti la Mwananchi, Ndg. Sharon Sauwa akiuliza shwari kwa Mtoa Mada (hayuko pichani) kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka gazeti la Uhuru, Ndg. Mussa Yusuph akiuliza shwari kwa Mtoa Mada (hayuko pichani) kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka Star TV, Ndg. Mozes Blaya akichangia jambo kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 
Mwandishi wa habari za Bunge kutoka Global TV, Ndg. Mohamed Zengwa akichangia jambo kwenye Mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma. 


Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali  Dkt.Hassan Abbasi akiwasilisha mada juu ya ‘Mambo Muhimu ya Kuzingatiwa na Waandishi wa Habari za Bunge’ kwenye mafunzo ya Waandishi wa habari za Bunge yaliyofanyika hii leo kwenye Ukumbi wa Msekwa-Bungeni Jijini Dodoma









Tuesday, November 24, 2020

SPIKA NDUGAI AWAAPISHA WABUNGE 19 WA VITI MAALUM WA CHADEMA JIJINI DODOMA

Wabunge Wateule wa Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA wakisubiri kula kiapo kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma 

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Matiko kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Bulaya kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Cecilia Pareso kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee akiongea jambo kwa niaba ya Wabunge wengine wa CHADEMA walioapishwa katika  Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma. 

SPIKA wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai katika picha ya pamoja na Wabunge wa Viti Maalum CHADEMA mara baada ya kuwaapisha. 


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai amewaapisha wabunge 19 wa viti maalum kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuwaapisha, Spika wa Bunge alieleza utaratibu wa kikatiba uliotumika kuwapata wabunge hao pamoja na utaratibu wa kikanuni wa kuwaapisha katika kipindi ambacho hakuna Mkutano wa Bunge.

Aidha, aliwaahidi wabunge hao kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila namna licha ya uchache wao Bungeni.

“Nawapongeza sana na mimi kama Spika jukumu langu ni kuwalinda walio wachache, hivyo naahidi kuwalinda na kuwapa ushirikiano wa kila hali wakati wa kutekeleza majukumu yenu,” alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake, Mheshimiwa Halima Mdee alimshukuru Spika kwa kuwapokea na kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuwatumikia Watanzania.

Waheshimiwa Wabunge waliokula kiapo ni Halima Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Esther Bulaya, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

 

Wengine ni Agnesta Kaiza, Nusrat Hanje, Asia Mohamed, Felister Njau na Stela Fiyao.

 

---------



Friday, November 20, 2020

MAFUNZO YA WAHESHIMIWA WABUNGE WA BUNGE LA 12 YAHITIMISHWA BUNGENI DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kushoto)  akihitimisha mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge wa Bunge la 12 leo Bungeni Dodoma. Katikati ni Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson na Kulia ni Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai.


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, (CAG) Ndg. Charles Kichere akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma. 


Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma.


Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Jaji (Mst.) Harold Nsekela akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma.


Katibu Mstaafu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge yaliyohitimishwa leo Bungeni Dodoma.


Mhasibu Mkuu-Ofisi ya Bunge, Ndg. Layson Mwanjisi akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge-Ofisi ya Bunge, Bi. Nenelwa Mwihambi akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge.

 

Mkurugenzi wa Idara ya Kamati za Bunge-Ofisi ya Bunge, Ndg. Athuman Hussein akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge.

 


 Mkurugenzi wa Idara ya Raslimali Watu-Ofisi ya Bunge, Bi. Jane Kajiru akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Waheshimiwa Wabunge.

 



Tuesday, November 17, 2020

MATUKIO KATIKA PICHA MAFUNZO YA WAHESHIMIWA WABUNGE YAKIENDELEA JIJINI DODOMA

Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai (katikati) akiongoza kikao cha mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge yanaoendelea  Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson  na kulia ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai.

Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson  akizungumza wakati wa  mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge yanaoendelea  Bungeni Jijini Dodoma. Kulia ni Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai.

Spika Mstaafu wa Bunge, Mhe. Pius Mswekwa akitoa mada wakati wa mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge yanaoendelea  Bungeni Jijini Dodoma.

 Spika Mstaafu wa Bunge, Mhe. Anne Makinda akitoa mada wakati wa  mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge yanaoendelea  Bungeni Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali, Wilbert Ibuge akitoa mada wakati wa  mafunzo ya Waheshimiwa Wabunge yanaoendelea  Bungeni Jijini Dodoma.

Waheshimiwa Wabunge wakiendelea na Mafunzo Bungeni Jijini Dodoma

 

Friday, November 13, 2020

RAIS DKT. MAGUFULI AHUTUBIA NA KUFUNGUA RASMI BUNGE LA 12



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akilihutubia na kulifungua rasmi Bunge la 12. Kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akilihutubia na kulifungua rasmi Bunge la 12. Kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai na kushoto ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia na kulifungua rasmi Bunge la 12.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. 

John Pombe Magufuli (katikati) na Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Bunge mara baada ya kulihutubia na kulifungua Bunge la 12 Wa pili kulia ni Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai, Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson (kushoto) na Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai

Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Afrika Masharikia, Martin Ngoga (kushoto) na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe. Zubeir Ali Maulid mara baada ya kumaliza ya ufunguzi wa Bunge la 12.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe

 John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Rais wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.

 John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia), Rais wa awamu ya Pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na Rais wa awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli (katikati) katika picha na Waheshimiwa Wabunge. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli (katikati) katika picha na Waheshimiwa Wabunge. 

Bofya hapa kusoma HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, WAKATI WA KUFUNGUA RASMI BUNGE LA 12 LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DODOMA, 13 NOVEMBA 2020 

Thursday, November 12, 2020

BUNGE LAMTHIBITISHA MHE. KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

Mpambe wa Rais akiingia Bungeni kuwasilisha bahasha yenye Jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Mhe. Rais kwa ajili ya kudhibitishwa na Bunge.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai akionesha kwa Waheshimiwa Wabunge bahasha yenye Jina la Waziri Mkuu mara baada ya kuipokea kutoka kwa Mpambe wa Rais.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai (kulia) na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai (katikati) wakifungua bahasha yenye Jina la Waziri Mkuu kutoka kwa Mheshimiwa Rais. Kushoto ni Mpambe wa Rais.

Spika wa Bunge, Mhe. Job Y. Ndugai (kulia) akitangaza  Jina la Waziri Mkuu mara baada ya kupokea bahasha yenye jina hilo kutoka kwa Mhe. Rais.

Mbunge wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kutangazwa  kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mbunge wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kutangazwa  kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


 Mbunge wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa akipongezwa na Waheshimiwa Wabunge mara baada ya kutangazwa  kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Mbunge wa Ruangwa, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza mara baada ya kudhibitishwa na Wabunge kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Bunge limemthibitisha Mbunge wa Jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa miaka mitano mingine (2020-2025) kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge sawa na asilimia 100.

    Akitangaza matokeo ya kura, Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema katika ya kura zote 350 zilizopigwa hakukuwa na kura ya hapana wala kura iliyoharibika.

    “Kura zote zilizopigwa ni 350 hakuna iliyoharibika, hakuna kura ya hapana. Kura zote 350 zimemthibitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, kwa hiyo ndugu wabunge Mheshimiwa Majaliwa amethibitishwa na Bunge hili kuwa Waziri Mkuu kwa kura 350 sawa na asilimia 100.

    Awali jina la Waziri Mkuu mteule liliwasilishwa Bungeni na Mpambe wa Rais na kukabidhiwa kwa Mheshimiwa Spika.

    Akizungumza baada ya kuthibitishwa Mheshimiwa Majaliwa amesema amepokea uteuzi huo kwa mikono miwili na anamshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kuwapa uhai wote na kushuhudia hayo, Pia amemshukuru Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa imani kubwa aliyoionesha juu yake.

    “Mheshimiwa Spika jambo hili si dogo, Mwenyezi Mungu ameliongoza, namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa imani kubwa aliyonayo juu yangu na kuendelea kuniamini. Namshukuru sana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ushiriki wake katika kuridhia jina langu.” Alisema.

    Mheshimiwa Majaliwa alimpongeza pia Mheshimiwa Spika kwa kuchaguliwa bila kupingwa kuwa mbunge wa Kongwa pamoja na kurudi katika nafasi yake ya uspika baada ya kupigiwa kura nyingi na waheshimiwa wabunge.

    Awali kabla ya kuthibitisha jina la Waziri Mkuu wabunge mbalimbali walizungumzia utendaji kazi wa Mheshimwa Majaliwa ambapo Mbunge wa Tunduma, Mheshimiwa David Silinde alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumrudisha tena Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika nafasi hiyo.

    Wabunge wengine waliopata fursa ya kumpongeza na kuzungumzia utendaji wake ni pamoja na Mheshimiwa William Lukuvi, Mheshimiwa Kapten Mstaafu George Mkuchika, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete, Mheshimiwa Fakharia Shomari na Mheshimiwa Januari Makamba.

 

DKT. TULIA ACHAGULIWA KUWA SPIKA WA BUNGE LA 12

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiapa mara baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12, Jijini Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza mara baada ya kuchaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12, Bungeni Dodoma.

   

 Bunge limechagua Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12.

Akitangaza matokeo hayo mara baada ya uchaguzi kufanyika, Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai alisema Dkt. Tulia amepata kura 350 kati ya kura 354 zilizopigwa.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, aliwashukuru Wabunge wote kwa ushindi huo wa kishindo na kuahidi kufanya nao kazi bega kwa bega bila kujali tofauti za kisiasa.

“Naahadi nitawatumikia, nitafanya kazi kwa ufanisi katika kazi zangu kama Naibu Spika, msisite kuniletea hoja zenu pale mnapukuwa nazo,” alisema

Aidha, alisema atamshauri vizuri Spika juu ya Sheria na Kanuni kwa kutumkia uzoefu alionao ili kuhakikisha haki inatendeka kwa wote.