WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, July 13, 2022

SPIKA DKT. TULIA AWAONGOZA WAJUMBE WA JUKWAA LA MABUNGE YA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA KUTOKA BUNGE LA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 51 WA SADC – PF NCHINI MALAWI














 Matukio katika Picha yaliyojiri leo Julai 13, 2022 wakati Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwaongoza Wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) kutoka Bunge la Tanzania katika Mkutano wa 51 wa SADC – PF unaoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Tuesday, July 12, 2022

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 51 WA SADC – PF




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akichangia mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika wakati wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi, leo Julai 12, 2022.

Katika Mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Jukwaa hilo kutoka Bunge la Tanzania ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymomd, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim.


Wajumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) kutoka Bunge la Tanzania wakishiriki katika Mkutano wa 51 wa SADC – PF wenye mada kuhusu mwelekeo wa upatikanaji wa nishati ya uhakika, endelevu na inayojitosheleza katika Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi, leo Julai 12, 2022. Kuanzia kushoto ni Mhe. Shally Raymond, Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim





 

SPIKA DKT. TULIA ACKSON ASHIRIKI MKUTANO WA 51 WA SADC – PF LILONGWE NCHINI MALAWI.











Matukio katika picha yaliyojiri wakati Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Katika Mkutano huo, Mhe. Spika ameambatana na Wajumbe wa Jukwaa hilo kutoka Bunge la Tanzania ambao ni Mhe. Selemani Zedi, Mhe. Shally Raymomd, Mhe. Hawa Mwaifunga, Mhe. Dkt. Alfred Kimea na Mhe. Haji Kassim.

 

SPIKA DKT. TULIA AKUTANA NA RAIS WA MALAWI JIJINI LILONGWE


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Mhe. Spika yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF).


 Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera (katikati) na Spika wa Bunge la Malawi, Mhe. Catherine Gotani Hara (kulia) walipokutana katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Bingu Jijini Lilongwe nchini Malawi.

Mhe. Spika yupo nchini humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF).

Sunday, July 10, 2022

SPIKA DKT. TULIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI POLEPOLE NCHINI MALAWI

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Malawi, Mhe. Humphrey Polepole baada ya kuwasili leo Julai 10, 2022 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu uliopo Lilongwe nchini humo.

Mhe. Spika atashiriki Mkutano wa 51 wa Jukwaa la Mabunge ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC – PF) utakaoanza tarehe 11 hadi 16 Julai, 2022 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Bingu (BICC) Jijini Lilongwe.





 

Friday, July 1, 2022

BUNGE WATEMBELEWA NA WAGENI MBALIMBALI KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

Maafisa wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Stergomena Tax alipotembelea Bunge katika viwanja vya sabasaba Jijini Dar-es-salaam.

Kaimu Balozi wa Jamhuri ya kislamu ya Iran Mhe. Hossein Alvandi Bahineh akisani kitabu cha wageni


Wanafunzi wa shule mbalimbali watembelea banda la Bunge liliopo katika viwanja vya sabasaba jijini Dar-es-salaam
 

Wednesday, June 29, 2022

SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI UFUNGUZI WA KONGAMANO MAALUM LA VIONGOZI WA DINI LA KUHAMASISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI.

 




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akifungua kongamano maalum la Viongozi wa dini la kuhamasisha sensa ya watu na makazi lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Juni 29, 2022 


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, pamoja na Spika Mstaafu wa Bunge, Mhe. Anne Makinda wakishiriki katika ufunguzi wa kongamano maalum la Viongozi wa dini la kuhamasisha sensa ya watu na makazi lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, leo Juni 29, 2022