Makamu Mwenyekiti wa
kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vicent Mbogo
akiongoza mazungumzo kati ya Wajumbe wa kamati hiyo (kushoto) na Mabalozi wa
Nchi za Umoja wa Ulaya (kulia) wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo, Mhe.
Manfredo Fanti (kulia) walipowatembelea leo tarehe 16 Septemba, 2022 Bungeni
Jijini Dodoma.
Friday, September 16, 2022
WAJUMBE KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA WAFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA BUNGENI JIJINI DODOMA
Thursday, September 15, 2022
SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA BUNGENI JIJINI DODOMA
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Manfredo Fanti pale ugeni kutoka Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo, Mhe. Manfredo Fanti (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akionyesha zawadi ya vitabu
alivyopewa na Balozi wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Manfredo Fanti pale ugeni wa
Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022
Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya
pamoja na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo,
Mhe. Manfredo Fanti (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 15 Septemba, 2022
Bungeni Jijini Dodoma.
Wednesday, September 14, 2022
SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU SPIKA WA PILI WA BUNGE LA GHANA, KIONGOZI WA UPINZANI BUNGE LA UGANDA
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Ghana,
Mhe. Andrew Amoako pale Wageni kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14
Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Naibu Spika wa Pili wa Bunge la Ghana,
Mhe. Andrew Amoako pale Wageni kutoka Bunge hilo walipomtembelea leo tarehe 14
Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wageni kutoka Bunge la Ghana wakiongozwa
na Naibu Spika wa Pili wa Bunge, Mhe. Andrew Amoako (kulia kwake) walipomtembelea
leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge Naibu
Spika wa Pili wa Bunge la Ghana, Mhe. Andrew Amoako pale Wageni kutoka Bunge
hilo walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Kiongozi wa Upinzani kutoka Bunge la Uganda,
Mhe. Mpuuga Mathias pale Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge hilo walipomtembelea
leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la
Uganda wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani wa Bunge, Mhe. Mpuuga Mathias (kulia
kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge,
Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi wa Upinzani kutoka
Bunge la Uganda, Mhe. Mpuuga Mathias pale Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge hilo
walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waheshimiwa Wabunge kutoka Bunge la Uganda wakiongozwa na Kiongozi wa Upinzani wa Bunge, Mhe. Mpuuga Mathias (kulia kwake) walipomtembelea leo tarehe 14 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.
Tuesday, September 13, 2022
SPIKA DKT. TULIA AMUAPISHA MHE. TAMIM HAJI ABASS
Mbunge Tamima Haji Abass akiapa kiapo cha uaminifu mbele ya Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa Mkutano wa Nane Kikao cha kwanza cha Bunge leo tarehe 13 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi
Monday, September 12, 2022
SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI JIJINI DODOMA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili
Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano
huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika
Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto kwake ni Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi
na Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu
Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Mussa Azzan Zungu akisoma maelezo ya
Spika kwa niaba ya Spika Dkt. Tulia Ackson wakati wa kikao cha kamati ya
uongozi kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na
Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika
Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
Katibu wa Bunge, Ndg. Nenelwa Mwihambi akishiriki kikao cha kamati
ya uongozi kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja
na Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba,
2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha kamati hiyo
kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na
Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika
Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma. Kuanzia kushoto ni Mhe. Joseph Mhagama,
Mhe. Najma Giga na Mhe. David Kihenzile
Wajumbe wa kamati ya uongozi wakiwa katika kikao cha kamati hiyo
kilichopokea na kujadili Shughuli za Mkutano wa Nane wa Bunge pamoja na
Mapendekezo ya Ratiba ya Mkutano huo leo tarehe 12 Septemba, 2022 katika
Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.
Friday, September 9, 2022
SPIKA DKT. TULIA MGENI RASMI HAFLA YA UTOAJI WA ZAWADI KWA WASHINDI WA INSHA YA KUPINGA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na Naibu
Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati alipowasili
katika hoteli ya St. Gasper Jijini Dodoma leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika
hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za
Utotoni. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule,
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe.
Stanslaus Nyongo (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la World Vision
Tanzania, Dkt. Diana Mndeme
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza jambo wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo
Dugange akizungumza jambo wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha
ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika
Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Wanafunzi Mbalimbali walioshiriki katika zoezi la uandishi wa
insha wakiwa katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga
Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akimkabidhi mfano wa hundi
ya Shillingi Million 1 Mwanafunzi Genoveva Mwakihwaja aliyeibuka Mshindi wa
kwanza katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga
Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi
wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais,
TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu kutoka Shirika la World Vision Tanzania na Wadau wa Maendeleo wakati wa hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa Insha ya Kupinga Ndoa na Mimba za Utotoni iliyofanyika leo tarehe 9 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa St. Gasper Jijini Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Afya), Mhe. Dkt. Festo Dugange (kushoto kwake), Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Stanslaus Nyongo (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la World Vision Tanzania, Dkt. Diana Mndeme (wapili kulia)
Thursday, September 8, 2022
WAJUMBE KAMATI YA PAC WAPOKEA MAELEZO KUHUSU MAJUKUMU YA OFISI YA MKAGUZI MKUU WA NDANI WA SERIKALI, WACHAMBUA TAARIFA YA HESABU ZILIZOKAGULIWA NA EWURA
Mwenyekiti wa
kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka
akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichokaa na Kupokea maelezo kuhusu majukumu
ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya
fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka
ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo tarehe 8 Septemba,
2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga
Mwenyekiti wa
kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati)
akiongoza kikao cha kamati hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu majukumu
ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya
fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka
ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) kilichofanyika leo tarehe 8 Septemba,
2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi
ya Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na
Maji (EWURA), Prof. Mark Mwandosya akijitambulisha mbele ya kamati ya kudumu ya
Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa na
kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali
katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya
Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) leo
tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Petroli EWURA, Ndg. Gerald Maganga na Mkurugenzi wa Fedha,
Utawala na Rasiliamali Watu EWURA, Ndg. Stanley Mahembe.
Mjumbe wa kamati ya
kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Isack Kamwelwe akichangia
jambo wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu
majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali katika udhibiti wa
matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na kuchambua Taarifa ya Hesabu
zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) leo tarehe 8
Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kamati
ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwa katika kikao cha kamati
hiyo kilichokaa na kupokea maelezo kuhusu majukumu ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali katika udhibiti wa matumizi ya fedha za Umma, Kupitia na
kuchambua Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na
Maji (EWURA) leo tarehe 8 Septemba, 2022 katika ofisi za Bunge Jijini Dodoma.