WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, October 3, 2022

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AMUAPISHA MBUNGE MTEULE MHE. ANGELLAH KAIRUKI JIJINI DAR-ES-SALAAM

Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiapa katika ofisi ndogo ya Bunge Jijini Dar-es-salaam.

Spikawa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) akishuhudia Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiweka saini mara baada ya kuapishwa katika ofisi ndogo ya Bunge Jijini Dar-es-salaam.



 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Tulia Ackson (Mb) amuapisha Mhe. Angellah Kairuki (Mb) aliyeteuliwa na Mheshimiwa Rais Mhe. Samia S. Hassan jana tarehe 02 Oktoba 2022

Wednesday, September 21, 2022

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA ZIMBABWE JIJINI DODOMA




Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Wabunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge hilo wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge, Mbunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambae pia ni Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire pale ugeni kutoka Bunge hilo ulipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge kutoka Bunge la Zimbabwe ambao pia ni Wajumbe wa kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia kwake) baada ya mazungumzo yaliyofanyika leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. 

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPAN NCHINI TANZANIA

Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.





Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akizungumza na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.



Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimpatia zawadi yenye mfano wa jengo la Bunge Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Tanzania ambaye pia ni Mwakilishi wa Japan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Yusushi Misawa alipomtembelea leo tarehe 21 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma. 

Tuesday, September 20, 2022

KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI, HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII ZAFANYA MAZUNGUMZO NA KAMATI YA AFYA NA HUDUMA KWA WATOTO KUTOKA BUNGE LA ZIMBABWE


Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Udhibiti wa dawa za kulevya na Ugonjwa wa Kifua kikuu, Mhe. Fatma Toufiq (katikati) akiongoza mazungumzo kati ya Wajumbe wa kamati hiyo, Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge la Zimbawe wakiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kanali Mstaafu Dkt. Joshua Murire (kulia) katika kikao kilichofanyika leo tarehe 20 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.





Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, Udhibiti wa dawa za kulevya na Ugonjwa wa Kifua kikuu pamoja na Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wafanya mazungumzo na kamati ya Afya na Huduma kwa Watoto kutoka Bunge la Zimbawe kikao kilichofanyika leo tarehe 20 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.

Friday, September 16, 2022

TIMU YA BUNGE SPORTS CLUB YAKABIDHIWA VIFAA VYA MICHEZO NA BENKI YA NMB


Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ndg. Ruth Zaipuna (kulia) amemkabidhi vifaa vya michezo Mwenyekiti wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Tarimba Abbas (wapili kulia) tukio lililofanyika leo tarehe 16 Septemba, 2022 katika Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya Bunge Sports Club, Mhe. Esther Matiko na Afisa wa Bunge, Ndg. Rai Karinga

Makabidhiano hayo ni kuelekea katika bonanza kati ya timu ya Bunge Sports Club na Benki ya NMB linalotegemewa kufanyika kesho tarehe 17 Septemba, 2022 katika viwanja vya Chinangali Jijini Dodoma.


WAJUMBE KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA WAFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA BUNGENI JIJINI DODOMA



 

Makamu Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vicent Mbogo akiongoza mazungumzo kati ya Wajumbe wa kamati hiyo (kushoto) na Mabalozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya (kulia) wakiongozwa na Balozi wa Umoja huo, Mhe. Manfredo Fanti (kulia) walipowatembelea leo tarehe 16 Septemba, 2022 Bungeni Jijini Dodoma.