Katibu wa Bunge
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi ofisi ya Bunge, Ndg. Nenelwa
Mwihambi, ndc akiongoza kikao cha
Baraza hilo kilichofanyika tarehe 20 Machi, 2024 katika ofisi za Bunge Jijini
Dodoma.
Thursday, March 21, 2024
KATIBU NENELWA AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE
Tuesday, March 19, 2024
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA MIRADI MITATU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA GEITA
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Munde Tambwe akizungumza kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya katika zahanati ya Bulela iliyopo Halmashauri ya Mji wa Geita, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati,Mheshimiwa Stansalaus Mabula na kushoto ni mjumbe wa Kamati hiyo Mheshimiwa Daimu Mpakate.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC),Mheshimiwa Stansalau Mabula akiambatana na wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua mradi wa ujenzi wa mpira wa miguu Geita katika Halmashauri ya Mji wa Geita.
Monday, March 18, 2024
KAMATI YA PAC YAKAGUA MRADI WA KUTOA MAJI ZIWA VIKTORIA NA KUSAMBAZA KATIKA MIJI YA TABOTA, IGUNGA NA NZEGA
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeridhishwa na utekelezaji wa mradi wa kupokea maji kutoka Ziwa Viktoria na kusambaza katika miji ya Tabora, Igunga na Nzega uliotekelezwa na Wizara ya Maji.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb) wakati Kamati ilipotembelea na kukagua mradi huo na baadae kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa awamu ya Kwanza na ya pili.
Alisema Kamati inaipongeza TUWASA kwa kusimamia vizuri mradi huo na kufikia malengo ya Serikali ya kufikisha maji safi na salama kwa wananchi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa ukame ambayo hayana vyanzo vya maji vya uhakika.
“TUWASA mmejitahidi sana, kwa macho tumejionea ubora wa miundombinu, sasa katika uendelevu wa mradi mlioueleza jitahidini na maeneo yaliyobakia ya Sikonge, Urambo Isikizya, kaliua, Shelui na Tinde maji yawafikie wananchi.” Alisema
Mheshimiwa Hasunga aliwasisitiza TUWASA kuhakikisha wanaongeza umakini na usimamizi wa miundombinu ya mradi huo kwa lengo la kuondoa kabisa changamoto ya upotevu wa maji ili wananchi wengi zaidi waweze kunufaika na mradi huo.
“Kwenye changamoto ya upotevu wa maji tutaendelea kupambana, ongezeni usimamizi ili maji yasipotee yawafikie wananchi.” Alisema
Mapema akiwasilisha taarifa ya Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Tabora (TUWASA) Mhandisi Mayunga Kashilimu amesema kukamilika kwa mradi huo kumewezesha wananchi zaidi ya milioni moja na laki mbili (1,200,000) wanapata huduma ya maji safi na salama.
“upatikanaji wa maji safi na salama umeongezeka hadi kufikia asilimia 100 katika Manispaa ya Tabora na miji ya Igunga, Nzega, Makao makuu ya Wilaya ya uyui pamoja na vijiji 102
Alisema huduma bora ya Maji inachangia kuboresha afya za wananchi wa maeneo husika na kuinua uchumi kupitia maendeleo ya sekta zingine zinazotegemea maji kama vile viwanda.
Kamati ya PAC, kesho inatarajia kukagua mradi wa kiwanda cha kupaka rangi mabomba kwa ajili ya kuweka mfumo wa upashaji joto mabomba katika mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga
Mwisho
KAMATI YA LAAC IMEKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA MKOANI KAGERA
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), akieleza jambo mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Manispaa hiyo katika Mkoa wa Kagera.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakiangalia msingi wa mojawapo ya jengo la Hospitali ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo potembelea na kukagua ujenzi wa hospitali hiyo katika Mkoa wa Kagera.
Sunday, March 17, 2024
KAMATI YA LAAC YATEMBELEA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISENYI NA SHULE YA SEKONDARI KITOBO KATIKA HALMASHAURI HIYO
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakikagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakikagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), akieleza jambo mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia mashine ya mionzi (x-rays) wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi.
Saturday, March 16, 2024
KAMATI YA LAAC YAKAGUA MIRADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akipima urefu wa msingi katika mojawapo ya jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa hospitali hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua ujenzi wa wa mradi wa Shule ya Sekondari Rukoma wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua ujenzi wa wa mradi wa Shule ya Sekondari Rukoma wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa na wajumbe wa Kamati, wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rukoma katika maabara ya somo la Kemia wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo iliyopo katika Hamashauri ya Wilaya ya Bukoba.
Friday, March 15, 2024
KAMATI YA LAAC YAKAGUA MIRADI MANISPAA YA KAHAMA
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakimsikiliza Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Lemburis Mollel akitaka ufafanuzi mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Dkt. Wilson Charles wakati wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.































