WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Monday, March 18, 2024

KAMATI YA LAAC IMEKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA MKOANI KAGERA



Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakiangalia msingi wa mojawapo ya jengo la Hospitali ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo potembelea na kukagua ujenzi wa  hospitali hiyo katika Mkoa wa Kagera

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakikagua mradi wa ujenzi wa Hospitali ya  Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi huo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), akieleza jambo mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa  Hospitali ya Manispaa hiyo katika Mkoa wa Kagera. 

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakiangalia msingi wa mojawapo ya jengo la Hospitali ya Manispaa ya Bukoba wakati Kamati hiyo potembelea na kukagua ujenzi wa  hospitali hiyo katika Mkoa wa Kagera. 






 

Sunday, March 17, 2024

KAMATI YA LAAC YATEMBELEA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISENYI NA SHULE YA SEKONDARI KITOBO KATIKA HALMASHAURI HIYO

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakikagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalus Mabula, wakikagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), akieleza jambo mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa  Hospitali ya Halmashauri hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), pamoja na wajumbe wa Kamati hiyo wakiangalia mashine ya mionzi (x-rays) wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi. 



 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari Kitobo   iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi. 

 

Saturday, March 16, 2024

KAMATI YA LAAC YAKAGUA MIRADI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOBA


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akipima urefu wa msingi katika mojawapo ya jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa hospitali hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua ujenzi wa wa mradi wa Shule ya Sekondari Rukoma  wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi  huo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

 

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakikagua ujenzi wa wa mradi wa Shule ya Sekondari Rukoma  wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi  huo uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba.

 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akiwa na wajumbe wa Kamati, wakiwasikiliza wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rukoma katika maabara ya somo la Kemia wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule hiyo iliyopo katika Hamashauri ya Wilaya ya Bukoba.

 

Friday, March 15, 2024

KAMATI YA LAAC YAKAGUA MIRADI MANISPAA YA KAHAMA

 

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakimsikiliza Mhandisi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama  wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Masud Kibetu akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Lemburis Mollel akitaka ufafanuzi mbele ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Dkt. Wilson Charles wakati wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mheshimiwa Stansalaus Mabula akitoa maelekezo kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama wakati Kamati hiyo ilipokuwa inakagua ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri hiyo.

 

Tuesday, February 13, 2024

SPIKA DKT. TULIA ACKSON AONGOZA WABUNGE KUSAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA WAZIRI MKUU MSTAAFU, HAYATI EDWARD NGOYAI LOWASSA BUNGENI JIJINI DODOMA.










Waheshimiwa Wabunge wakiongozwa na Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, Mhe. Dkt. Tulia Ackson wamesaini kitabu cha maombolezo ya Waziri Mkuu Mstaafu, Hayati Edward Ngoyai Lowassa, tarehe 13 Februari, 2024 Bungeni Jijini Dodoma.







 

Wednesday, January 31, 2024

SPIKA DKT. TULIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA AZANIA JIJINI DODOMA

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Ndg. Esther Mang’enya alipotembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 31 Januari, 2024.

 

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia ameipongeza Benki hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikishiriki vyema katika kusaidia jamii na kuongeza kasi ya maendeleo nchini.


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania, Ndg. Esther Mang’enya alipotembelea ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 31 Januari, 2024. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki hiyo, Dkt. Rhimo Nyansaho.

 

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia ameipongeza Benki hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikishiriki vyema katika kusaidia jamii na kuongeza kasi ya maendeleo nchini.


Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Benki ya Azania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ndg. Esther Mang’enya (wa pili kushoto) baada ya mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo tarehe 31 Januari, 2024.

 

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia ameipongeza Benki hiyo kwa namna ambavyo imekuwa ikishiriki vyema katika kusaidia jamii na kuongeza kasi ya maendeleo nchini.

 

 

SPIKA DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI BUNGENI JIJINI DODOMA


















Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiongoza kikao cha kamati ya uongozi kilichopokea na kujadili mapendekezo ya ratiba ya Mkutano wa kumi na nne wa Bunge kilichofanyika katika Ukumbi wa Spika Bungeni Jijini Dodoma.