WELCOME TO TANZANIA NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL BLOG: CONTACT US: P.O.BOX 941 DODOMA, TANZANIA, WEBSITE: parliament.go.tz , FIND US ON FACEBOOK >>> www.facebook.com/bungetz1, FOLLOW US ON TWITTER >>> @bunge_tz.>>>KARIBUNI

Wednesday, October 31, 2018

KAMATI YA SHERIA NDOGO YAKUTANA NA WATENDAJI WA WIZARA YA FEDHA

   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt Ashatu Kijaji na  Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipanfo Ndg. Elias Kalist  wakiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo walipopeleka majibu ya Serikali yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge la Kumi na Moja leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.


   Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo Mheshimiwa William Ngeleja akisisitiza jambo wakati Kamati yake ilipokutana na Wizara ya Fedha na Mipango  kupokea na kujadili majibu ya Serikali yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge la Kumi na Moja leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

       Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo wakiendelea na majadiliano wakati Kamati hiyo ilipokutana na Wizara ya Fedha na Mipango kupokea na kujadili majibu ya Serikali yatokanayo na Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge la Kumi na Moja leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma.

KAMATI YA KATIBA NA SHERIA YAENDELEA NA VIKAO JIJINI DODOMA

    Naibu waziri wa Elimu,  Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Tate William Ole-Nasha  akitoa Taarifa ya Wizara ya Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Mkakati wa Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria leo katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Mheshimiwa Ole-Nasha alimuwakilisha Waziri wa Katriba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi.
 
   Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakimsikiliza Naibu waziri wa Elimu,  Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Mheshimiwa Tate William Ole-Nasha  akitoa Taarifa ya Wizara ya Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Mkakati wa Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka leo katika Ofisi za Bunge, Jijini Dodoma.  

      Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mheshimiwa Najima Giga akifurahi jambo wakati kamati hiyo ilipokutana na Wizara ya Katiba na Sheria kupokea na kujadili  Taarifa ya Wizara ya Wizara hiyo kuhusu Mkakati wa Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka. Kushoto kwa Mheshimiwa Giga ni katibu wa Kamati hiyo Ndg. Kagisa.

Tuesday, October 30, 2018

KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YAKUTANA NA WIZARA YA ULINZI

Mwenyekiti wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Mussa Azan Zungu akifuatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  iliyowasilishwa na Meja Jenerali A. Bahati mbele ya Kamati Bungeni Jijini Dodoma

  Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Alli Mwinyi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Florens Turuka  wakiwa mbele ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wizara hiyo ilipoenda kuwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019.

Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama  pamoja na  Watendaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  wakifatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  iliyowasilishwa na Meja Jenerali A. Bahati (hayupo pichani)  mbele ya Kamati Jijini Dodoma

   Wajumbe wa Kamati ya ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama  na Watendaji wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  wakifatilia uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018  iliyowasilishwa na Meja Jenerali A. Bahati mbele ya Kamati Bungeni Jijini Dodoma

KAMATI YA MIUNDOMBINU YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA UJENZI WA SGR


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Selemani Moshi Kakoso ilyokutana na Shirika la Reli nchini TRC hii leo Jijini Dodoma na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Reli ya mpya ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Injinia Isack Aloyce Kamwelwe akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokutana na Shirika la Reli nchini TRC hii leo Jijini Dodoma na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Reli ya mpya ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mheshimiwa Selemani Moshi Kakoso akifafanua jambo mbele ya Kamati hiyo ilipokutana na Shirika la Reli nchini TRC hii leo Jijini Dodoma na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Reli ya mpya ya Kiwango cha Kimataifa (SGR).

Monday, October 29, 2018

KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA IKIWA KATIKA KIKAO CHA KAMATI JIJINI DODOMA

Kamati ya Bunge ya Utawala  na Serikali za Mitaa ikiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo imekutana na  Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais , Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma. 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mhe. Mwanne Nchemba akisisitiza jambo katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma. Kamati hiyo imekutana na  Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais , Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. George Mkuchika akitolea ufafanuzi hoja za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakati Kamati hiyo ilipokutana na Wizara yake  kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais , Bodi ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma

KAMATI YA MADINI YAENDELEA NA VIKAO JIJINI DODOMA

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ikiwa katika kikao cha Kamati kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ambapo imekutana na Wizara ya Madini kwa ajili ya kupokea na kujadili taarifa ya Wizara hiyo  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Madini Ndugu Augustine Ollal akiwasilisha taarifa ya Wizara hiyo  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 katika kikao cha Kamati ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Oofisi za Bunge Jijini Dodoma. Wengine ni manaibu Mawaziri wa Wizara hiyo, Mhe. Stanslaus Nyongo (katikakati) na Mhe. Doto Biteko.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati  na Madini Mhe. Mariam Ditopile akifuatilia uwasilishwaji wa taarifa  Wizara ya Madini  kuhusu upatikanaji wa fedha za miradi ya maendelepkatika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2018/19 katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.pembeni yake ni Katibu wa Kamati hiyo Ndugu Felister Mgonja.


Tuesday, October 23, 2018

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA ATEMBELEA MIRADI YA UJENZI YA OFISI YA BUNGE INAYOTEKELEZWA NA SUMA JKT

    Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakisikiliza maelezo kutoka kwa  Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge wakati viongozi hao walipotembelea eneo linapojengwa lift katika Jengo la Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma . 
        Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai akizungumza na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Dodoma. Waziri mwinyi ametembelea Ofisi ya Bunge kukagua miradi mitatu 3 ya ujenzi ya inayotekelezwa na Suma JKT.


       Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Hussein Ally Mwinyi wakimsikiliza Mkuu wa SUMA-JKT – Ujenzi Kanda ya Kati Dodoma, Luteni Kanali Zabron Mahenge akitoa maelezo ya hatua ya utekelezaji mradi wa ukarabati wa Ofisi ya Bunge ulipofikia. Nyuma ya Waziri Mwinyi (mwenye miwani ) ni Mkurugenzi Mtendaji SUMA JKT Kanali Rajab Mabere na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT Meja Jenerari Martin Busungu .



Friday, October 19, 2018

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA BUNGE LA CHINA


Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza na Mgeni wake Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) alipomtembelea hii leo na kufanya nae mazungumzo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akimvalisha vazi la Kimasai mgeni wake ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei kama ishara ya Utamaduni wa Kitanzania walipokutana na kufanya mazungumzo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma hii leo.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Wang Ke alipomtembelea na kufanya nae mazungumzo hii leo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma. Balozi huyo aliambatana na ujumbe kutoka Bunge la China ulioongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei.
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na Wageni kutoka China wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei (kulia kwa Spika) walipokutana hii leo kwenye Ukumbi wa Spika Jijini Dodoma, kushoto kwa Spika ni Balozi wa China hapa nchini Mheshimiwa Wang Ke. Baadhi ni Watumishi wa Ofisi ya Bunge.
Wageni wa Mheshimiwa Spika kutoka nchini China wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge la China (CPPCC) Mheshimiwa Prof. Lou Jiwei wakipewa maelekezo kuhusiana na mpangilio wa ukaaji Bungeni kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki na Uhusiano wa Kimataifa – Ofisi ya Bunge, Ndg. Daniel Eliufoo walipotembelea Bungeni Jijini Dodoma hii leo.