Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akikabidhi mifuko 200 ya saruji kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
Itezi, Ndg. Betseba Nsemwa ikiwa ni mchango wake kwa Shule hiyo tukio
lililofanyika leo Mkoani Mbeya,
Februari 28, 2022, Kushoto
ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dormohamed Rahmat na kulia ni Diwani wa
kata ya Itezi, Mhe. Sambee Shitambala wengine ni Vijana kutoka Taasisi ya Tulia
Trust
Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akisalimiana na wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Itezi wakati alipowasili Shuleni hapo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022, kulia mbele ni Diwani wa kata ya Itezi, Mhe.
Sambee Shitambala
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na wananchi na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itezi (hawapo kwenye picha) wakati alipoitembelea Shule hiyo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022, kushoto ni Mbunge wa Mchinga, Mhe. Salma Kikwete na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, Mhe. Dormohamed Rahmat
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Itezi wakimsikiliza
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akizungumza wakati alipoitembelea Shule hiyo leo Mkoani Mbeya, Februari 28, 2022
Wananchi Mbalimbali
wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt.
Tulia Ackson, akizungumza katika viwanja vya Shule ya Sekondari Itezi wakati
alipoitembelea Shule hiyo leo Mkoani Mbeya,
Februari 28, 2022