Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa kwanza kushoto) akiongoza kikao cha Bodi ya
Uwekezaji ya Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya
Afrika kilichofanyika katika Hotel ya Manidat AL Bahr Business and Spa Hotel. Katikati ni Katibu wa CPA Kanda ya Afrika,
Ndugu Stephen Kagaigai na Ndugu Said Yakubu Katibu Msaidizi wa CPA Afrika
Saturday, August 31, 2019
NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA NAIBU SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA AFRIKA YA KUSINI
Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiwa pamoja na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa Tsenoli wakifurahia dafu wakati walipotembelea shamba la viungo (Spice farm) visiwani Zanzibar. Viongozi hao wapo visiwani humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika.
|
Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akipewa zawadi ya bangili wakati
yeye na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Afrika ya Kusini, Mhe. Lechesa
Tsenoli walipotembelea shamba la viungo (Spice farm) visiwani Zanzibar. Viongozi hao wapo visiwani
humo kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 50 wa Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya
Madola (CPA), Kanda ya Afrika.
Friday, August 30, 2019
SPIKA WA BUNGE, MHE.JOB NDUGAI AWASILI ZANZIBAR
SPIKA WA BUNGE LA LESOTHO AWASILI ZANZIBAR KUHUDHURIA MKUTANO WA CPA
Spika wa Bunge la Lesotho, Mhe. Sephiri Enoch Motanyane akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar. |
Spika wa Bunge la Lesotho, Mhe. Sephiri Enoch Motanyane akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar Chumba cha mapumziko na wenyeji wake. |
Thursday, August 29, 2019
SPIKA WA BARAZA LA WAWAKILISHI AKAGUA MAANDALIZI YA MKUTANO WA CPA
Spika wa Bunge la Baraza la Wawakilishi Mheshimiwa Zubeir Ali
Maulid amewataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kutumia fursa waliyoipata
ya kuwa wenyeji wa Mkutano wa 50 wa
Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Kanda ya Afrika kujitangaza kibiashara na
kitalii.
Mheshimiwa Maulid ametoa rai hiyo leo Kisiwani Zanzibar
wakati akikagua maandalizi ya Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe
30 Agosti hadi septemba 5 mwaka huu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Business
& Spa.
Alisema mkutano huo kufanyika Zanzibar utafungua fursa katika
sekta za biashara ikiwemo utalii na kuwataka Watanzania kuonyesha ukarimu kwa
wageni hao.
“Tuonyeshe ukarimu wakati kupokea wageni hawa, tuitendee haki
nchi yetu, tukikaa nao vizuri wageni wetu itatosha kwa sisi kujitangaza,
tutumie fursa hii kwa kadri tutakavyoona inaweza kuisaidia nchi” alisema.
Alisema mkutano huo ni wa kihistoria kwa kuwa unaweza kuvunja
rekodi ya mahudhurio ya wajumbe zaidi ya 400 kutoka nchi 18 wanachama ambao unajumuisha
maspika, manaibu spika na wabunge.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CPA, Tawi la Zanzibar, Mheshimiwa
Simai Mohammed Said alisema mkutano huo mbali na kutoa fursa za kiuchumi lakini
pia utawezesha wajumbe kubadilishana uzoefu wa jinsi ya kutekeleza majukumu yao
ikiwemo kuisimamia Serikali katika mambo yanayogusa wananchi.
Awali akizungumzia maandalizi ya awali, Katibu Msaidizi wa
CPA, Kanda ya Afrika, Said Yakubu alisema Nchi zote 18 wanachama zimethibitisha
ushiriki na kwamba maspika 23 kutoka mabunge makubwa na madogo watahudhuria.
Alisema nchi wanachama wa CPA, Kanda ya Afrika ni Botswana,
Cameroon, Eswatini, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji,
Namibia, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Siera – Leone, Afrika ya Kusini,
Tanzania, Uganda na Zambia.
SPIKA WA BUNGE MHESHIMIWA JOB NDUGAI AKARIBISHA USHIRIKIANO NA NCHI YA IRELAND
Spika wa Bunge Mheshimiwa, Job Ndugai ameishukuru Serikali ya
Ireland kwa kuendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya sheria
na haki za binadamu.
Mheshimiwa
Spika ametoa shukrani hizo leo ofisini kwake Bungeni JIjini Dodoma
wakati alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria wa haki za binadamu kutoka
Ubalozi wa Ireland wakiongozwa
na Naibu Balozi wa Ireland hapa nchini Mheshimiwa Bronagh Carr.
Alisema
Tanzania itaendelea kudumisha ushirikiano huo na Serikali ya Ireland
katika masuala hayo ya sheria pamoja na kudumisha haki za binadamu.
Aidha,
alisema upo umuhimu
ujumbe huo, ukakutana na Umoja wa Wabunge Wanawake nchini (TWPG) ili
kujadili
changamoto za kijinsia zilizopo katika maeneo yao na kuzitafutia
ufumbuzi kwa kuwa Ireland imepiga hatua kubwa kwenye masuala ya usawa wa
kijinsia.
aliwataka pia wakutane na Kamati
ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambapo miswada yote
inayoathiri huduma za jamii ikiwemo masuala ya elimu na jinsia hujadiliwa
kwenye kamati hiyo kabla ya kuingia Bungeni.
“Katika suala la usawa kwa jinsia Bunge letu limepiga hatua kubwa
ambapo Wabunge wa Viti Maalum Wanawake ni asilimia 30 ya Wabunge
wote 393 pia wapo Wabunge wa majimbo ambao ni Wanawake hivyo kuongeza nafasi ya
uwakilishi wa jinsi hiyo Bungeni” alisema Mheshimwa Spika.
kwa upande wake Kaimu Balozi wa Ireland, Mheshimiwa Bronagh Carr
alimshukuru Mheshimiwa Spika kwa kukubali kukutana nae pamoja na Kamati za Bunge.
Alisema ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland umekuwepo kwa kipindi cha miaka
40 na unazidi kuimarika siku hadi siku.
Ujumbe huo umelenga kukutana na wadau mbalimbali wa masuala ya
kisheria ikiwemo Wabunge, Mwendesha mashitaka mkuu wa Serikali
pamoja na Jeshi la polisi nchini ili kuimarisha ushirikiano katika masuala ya
sheria na jinsia.
Spika
wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akisalimiana na Naibu Balozi wa Ireland
hapa nchini walipokutana na kufanya mazungumzo Ofisini kwake Bungeni
Jijini Dodoma hii leo.
|
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akifafanua jambo alipokutana na Ujumbe wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo. |
Spika wa Bunge Mheshimiwa Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Wanasheria kutoka ubalozi wa Ireland nchini waliomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma hii leo. |
Friday, August 23, 2019
KATIBU WA BUNGE ATEMBELEWA NA JAJI MFAWIDHI WA MAHAKAMA KUU KANDA YA DODOMA
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen
Kagaigai akizungumza na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe.
Lameck Mlacha wakati Jaji huyo alipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jjijini Dodoma.
|
Thursday, August 22, 2019
Tuesday, August 20, 2019
WAJUMBE WA KAMATI YA BAJETI WAKIWA KATIKA KIKAO
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma |
|
Afisa Bajeti kutoka Ofisi ya Bunge, Maombi Kakozi akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti katika kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma |
WAJUMBE WA KAMATI YA NISHATI WAPOKEA TAARIFA YA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI MIRADI YA REA
KAMATI YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA YAJADILI MUSWADA WA SHERIA YA SERIKALI MTANDAO WA MWAKA 2019
Saturday, August 17, 2019
Friday, August 16, 2019
KAMATI YA PAC YAPEWA MAFUNZO NA OFISI YA MSAJILI WA HAZINA
Mkurugenzi wa Uwekezaji kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina Ndg. Lightness Mauki akifafanua jambo alipokuwa akitoa Mada kuhusu Changamoto za usimamizi wa Matumizi ya Mashirika ya Umma nchini kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali PAC iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma hii leo.
|
Thursday, August 15, 2019
BARAZA LA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE LANDELEA NA KIKAO
Wednesday, August 14, 2019
SPIKA WA BUNGE AWATAKA WAFANYAKAZI WA OFISI YA BUNGE KUFANYA KAZI KWA BIDII
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
amewataka watumishi wa Bunge kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa bidii.
Mhe. Spika alitoa rai hiyo kupitia
hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Spika, Mhe. Dkt. Tulia Ackson alipokuwa
anazindua Baraza la Wafanyazi la Ofisi ya Bunge lililofanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge Tunguu Zanzibar.
Alisema kunahitajika mabadiliko
katika utekelekezaji wa majukumu ya kila siku kwa watumishi katika kuchapa kazi
ili kuleta utendaji kazi wenye tija na ufanisi.
Aidha, aliwataka wajumbe kupitia
mada zitakazowasilishwa katika Mkutano huo wa Baraza kukumbuka wajibu wao
katika kutelekeza majukumu waliyopewa kulingana na taaluma husika na hatimaye
kufanikisha utekelezaji bora wa majukumu na madaraka ya Bunge Kikatiba.
Vilevile, alimpongeza Katibu wa
Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai kwa kufanikisha utatuzi wa changamoto ya muda
mrefu ya muundo wa Ofisi ya Bunge ambayo hatimaye ufumbuzi umewezesha kuundwa
kwa Baraza la Wafanyakazi.
“Naomba
nitumie fursa hii kuwapongeza watumishi wote mlioteuliwa na Tume ya Utumishi wa
Bunge kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi na ni matumini yangu kwamba
mtatumia uwezo na karama mlizojaaliwa na Mwenyezi Mungu katika kutekeleza
majukumu yenu kwa ufanisi hivyo kuliwezesha Bunge kufikia malengo yake,” alisema.
Aliwapongeza pia Wajumbe na Wawakilishi
wa Idara na Vitengo kwa kuchaguliwa kushika nafasi hizo na kuwataka kutumia
nafasi zao ili kuwa kiungo kati ya Wafanyakazi wa kada, ngazi zote, Menejimenti
na Tume ya Utumishi wa Bunge.
Uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi
ulihudhuriwa na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na
Afya, TUGHE Ndugu Hery Nkunda na Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma Ndugu John Mchenya
ambao walinasihi Baraza kudumisha ushirikiano na kuongeza ufanisi katika ujenzi
wa nchi.
Awali akizungumza katika mkutano
huo, Katibu wa Bunge Ndugu Stephen Kagaigai alisema Ofisi ya Bunge imeunda
Baraza la Wafanyakazi baada kutokuwepo ya Baraza hilo katika kipindi kirefu
kutokana na changamoto zilizokuwepo za kimuundo za Ofisi ya Bunge.
Alisema, lengo la Baraza lililopo
kisheria ni kuboresha utendaji kazi wa
taasisi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na bila ya ugomvi wala mifarakano.
Kabla ya uzinduzi wa Baraza la
Wafanyakazi, wajumbe walimchagua Ndugu Frank Mbilinyi kuwa katibu wa Baraza na
Ndugu Felister Njovu kuwa Katibu
Msaidizi.
NAIBU SPIKA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA BUNGE
Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano wa
Wafanyakazi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo
za Bunge, Tunguu Zanzibar pamoja na Ndugu Chacha Nyakega Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Ofisi ya Bunge na Ndugu Triphonia
Mng’ong’o Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu.
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo
za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge uliofanyika katika Ofisi Ndogo
za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi Katibu wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai Mkataba kwa ajili ya kuunda
Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo.
Uzinduzi huo umefanyika katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Ndugu Hery Nkunda Mkataba kwa ajili ya
kuunda Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge baada ya uzinduzi. Uzinduzi huo umefanyika
katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akimkabidhi Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa wa Dodoma , Ndugu John Mchenya Mkataba kwa ajili ya kuunda Baraza la
Wafanyakazi la Ofisi ya Bunge mara baada ya kuzindua Baraza hilo. Uzinduzi huo umefanyika
katika Ofisi Ndogo za Bunge, Tunguu Zanzibar
|
Wajumbe wa Baraza wakiwa katika picha ya pamoja |
Subscribe to:
Posts (Atom)